MWANAUME mmoja aliyeelezwa kuwa ni tajiri mwenye nazo mjini, amezua
tafrani na kusababisha timbwili la nguvu kwa dakika kadhaa baada ya
kugonganisha wanawake wawili waliodaiwa kuwa chini ya miliki yake kwa
wakati mmoja, subiri hapohapo tukujuze!
Mtiti
huo uliovuta hisia za wengi ulichukua nafasi Ijumaa iliyopita, mishale
ya saa sita na dakika zake usiku, pande za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere ‘JNIA’ ambapo mwanaume huyo ambaye jina lake
halikupatikana mara moja alitua na Ndege ya Shirika la Kenya.
ANGALIA SINEMA
Hali ya hewa ilikuwa ya kuridhisha kabisa katika eneo la uwanja wa ndege wakati paparazi wetu akiwa kwenye sehemu maalum ya kusubiria abiria wanaotua uwanjani hapo wakitokea nje ya nchi.
Paparazi wetu alikuwa akimsubiri mgeni wake lakini kama ilivyo kawaida ya wanakikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ alikuwa na zana zake za kazi kama kawaida.

Wakati
wageni wakianza kutoka, ghafla zilisikika kelele pembeni mwa sehemu
aliyokuwa paparazi wetu, akajiuliza kunani? Akaweka zana zake za kazi
sawa kisha akajongea eneo la tukio.
VARANGATI LA NGUVU
Kamera za Risasi Mchanganyiko zilishuhudia wanawake wawili wakikunjana na kupigana makonde huku mmoja akimshutumu mwenzake kumwibia mumewe (haikujulikana kama ni wa ndoa). Alisema: “Wewe mpumbavu mwizi wa waume za watu, nitakukomesha leo. Si umezoea kuiba waume za watu? Sasa utanijua mimi ni nani?”

Mwanamke
huyo aliyeonekana kuwa na jazba, alikuwa na watoto wake wawili
waliovalia sare za shule ambao walikuwa wakimvuta na kumsihi aachane na
ugomvi.
MSHANGAO NI HUU!
Sekeseke wakati likiendelea, yule mwanamke ambaye alikuwa akidai kuibiwa mumewe kwa muda mrefu na mwanamke huyo, watoto wake wawili walikuwa naye sambamba huku wakijaribu kumtuliza ingawa kiumri ni wadogo.
Mwanamke aliyedaiwa kuchukua mume wa mwenzake naye alikuwa na mtoto wake mmoja ambaye alikuwa akimvuta akitaka kumtoa mikononi mwa mwanamke aliyedaiwa kuwa mmiliki rasmi wa tajiri huyo.

Mshangao
mkubwa ni kitendo cha watoto hao wote kuwa wamevaa sare za shule, tena
zikionekana kuwa za shule moja – maswali yalikuwa mengi kuliko majibu!
“Hawa watoto sijui wamekuja na huyu jamaa? Maana wanaonekana kama wanasoma shule moja na wapo na vifaa vyao vyote vya shule. Hapa hata haileweki jamani,” alisikika dereva teksi mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.

MAELEZO MENGINE
Mashuhuda walisema, awali tajiri yule wakati anatoka katika sehemu maalum ya abiria wanaoingia nchini, alikimbiliwa na mwanamke yule anayedaiwa kuwa kimada na kumpokea kisha kumbusu na kumpa pole kwa safari.

“Tatizo lilianzia pale yule mwanamke mwembamba mwenye nguo nyekundu
alipoenda kumpokea jamaa. Alimfuata na kumkumbatia kisha akambusu, basi
hapo tafrani ikatokea. Yule mke wa jamaa alikwenda haraka na kumvamia
kisha kuanza kumpiga,” alisikika mmoja wa mashuhuda hao.
TAJIRI AWAZODOA WALIOMSHANGAA!
Wakati tafrani ile ikiendelea, mwanaume huyo aliwaingilia kati na kuwaamulia, jambo lililozidisha watazamaji wa sinema hiyo ya bure kushangaa.

Katika hali ya kushangaza, tajiri huyo aliwananga watu waliokuwa
wakimshangaa akisema: “Sasa kipi cha ajabu? Ni mwanaume gani hapa ambaye
hajawahi kufumaniwa? Haya ni mambo ya kawaida, endeleeni na shughuli
zenu nitamaliza hii ishu mwenyewe.”
Juhudi
za tajiri huyo kuwaachanisha zilizaa matunda, kwani zaidi ya kutumia
nguvu, alionesha ‘uanaume’ wake kwa wanawake hao ambao walikubali
kuachana na ugomvi huo ingawa kila mmoja alionekana kuwa na hasira na
mwenzake.
Baadaye yule mwanamke aliyedaiwa kuwa ndiye mke halali wa tajiri yule,
aliondoka naye wakiwa na watoto wao wawili, mwingine akaondoka na mtoto
wake.
CREDIT-GPL
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako