A

A

MTOTO WA MIAKA 12 ANASWA AKIJIUZA JIJINI MWANZA

Hii ni aibu kwa taifa! ‘Makachero’ wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) iliyo chini ya Global Publishers wameibua uozo mwingine jijini Mwanza baada ya kubamba tukio la kusikitisha na kufedhehesha la mtoto mwenye umri wa miaka 12 akijiuza.
Uchunguzi wa OFM jijini hapa wiki iliyopita umebaini kuwa vitendo hivyo vinaonekana vya kawaida na kuzoeleka miongoni mwa wakazi wake, jambo linalotia dosari kwa mji huo unaosifika kwa usafi wa hali ya juu wa mazingira.
OFM ilishuhudia wimbi kubwa la watoto wa kike walio chini ya umri wa miaka 18 wakijihusisha na biashara haramu ya kuuza miili nyakati za usiku.
Awali taarifa za uwepo wa watoto hao jijini Mwanza zilipokelewa katika ofisi za Global Publishers jijini Dar kutoka kwa baadhi ya wasafiri na wakazi wa jiji hilo wakiomba kupelekwa kwa OFM kutokana na suala hilo kutofanyiwa ufumbuzi na taasisi husika.

“Jamani hii ni aibu kwa taifa letu! Hapa Mwanza mjini kuna vibinti vidogo sana vinauza miili, tunaomba OFM isibakie Dar pekee, njooni na huku hali inatisha,” aliomba mkazi mmoja wa Mwanza.
OFM huwa haipuuzi taarifa kutoka kwa vyanzo vyake hivyo iling’oa nanga katika jiji la maraha na karaha la Dar na kutinga rasmi Jiji la Miamba (Rocky City) Mwanza kufanyia kazi kilichosemwa.
Kweli watoa taarifa walikuwa na hoja kwani katika viunga vya Mwanza Mjini maeneo ya Kauma jirani na Mnara wa Samaki kwenye Barabara ya Nyerere, OFM iliwashuhudia watoto hao wakijiuza bila wasiwasi huku wakilindwa na watoto wenzao wa jinsia ya kiume waliokuwa na chupa na viwembe kama silaha zao.
Katika utafiti wake, mmoja wa ‘makamanda’ wa OFM alijifanya mteja kwa watoto hao ambapo alifanikiwa kuongea nao.
Kuhusu bei, mmoja alieleza kuwa huwa wanatoza shilingi 20,000 kwa kulala usiku mzima na elfu 5,000 kwa short time.
Maskini! Mtoto Aisha (12) alikuwa yupo tayari kuchukuliwa kwa makubaliano yoyote ambapo alisema kinachomfanya kujihusisha na biashara hiyo ni hali ngumu ya maisha na wazazi wake kushindwa kumsomesha.
Katika kazi hiyo ya OFM jijini Mwanza, mtoto huyo alidai kuwa alipopelekwa shule ya msingi huko wilayani Sengerema, wazazi wake walishindwa kumudu michango ya kila kukicha hivyo akabaki nyumbani hadi alipotorokea jijini.
Akizungumza na OFM juu ya sakati hilo la kushamiri kwa biashara hiyo haramu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alisema: “Sina taarifa yoyote kuhusiana na watoto hao wanaojiuza ndiyo nasikia labda nipate muda wa kuzungumza na uongozi wa chini nitalichukulia hatua mara moja.”

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako