A

A

STARS...ILIVYOKUWA RAHA LEO MOMBASA WAKIMVUA UBINGWA UGANDA CHALLENGE

Wachezaji wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kutoka kulia, Michael Aidan, Athumani Iddi 'Chuji', Thomas Ulimwengu na Frank Domayo wakikimbia kumfuata kipa Ivo Mapunda baada ya kucheza penalti ya mshambuliaji wa Uganda, Dani Sserunkuma na kuipa Stars ushindi wa penalti 3-2, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90, Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya hivyo kutinga Nusu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.  

Godfrey Kizito wa Uganda kulia akipambana na Thomas Ulimwengu wa Stars

Ivo Mapunda akicheza penalti ya Dani Sserunkuma

Mrisho Ngassa akitafuta mbinu za kumtoka Godfrey Kizito 

Salum Abubakar 'Sure Boy' akimtoka Hamisi Kiiza wa Uganda

Mbwana Samatta akimlamba chenga Nico Wadada wa Uganda

Nahodha wa Stars, Kevin Yondan akiwapa ishara mashabiki baada ya kufunga penalti ya mwisho

Martin Mpouga wa Uganda, akimdhibiti Thomas Ulimwengu wa Stars

Mrisho Ngassa akitafuta njia za kuwatoka mabeki wa Uganda

Thomas Ulimwengu wa Stars akimgeuza Kasaga Richard wa Uganda

Wakosa penalti; Mbwana Samatta kulia na Erato Nyoni kushoto wakisikitika baada ya kukosa penalti 

Godfrey Walusimbi akimziba Mrisho Ngassa ili mpira utoke nje

Unawabeba sana Waganda; Mrisho Ngassa akilalamika jambo kwea refaWish Yabarow kutoka Somalia, huku Emmanuel Okwi wa Uganda akimuangalia

Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Stars akigombea mpira na Emmanuel Okwi wa Uganda kushoto

Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa Uganda

Mbwana Samatta akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Uganda, 

Samatta akitafuta njia za kumtoka beki wa Uganda Godfrey Kizito 

Kikosi cha Stars leo

Kikosi cha Uganda

Shabiki maarufu wa Tanzania, Ally akiishangilia Stars leo Mombasa

Moja kwa moja hadi Kampala; Kocha wa Uganda, Mserbia, Milutin Sredojevic 'Micho' kulia akiondoka uwanjani baada ya mechi. Uganda inarejea Uganda baada ya kutolewa na Stars leo

Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Malota Soma 'Ball Juggler' alikuwepo uwanjani leo kuisapoti Stars 

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Iddi Moshi 'Nyamwezi' alikuwepo pia tena na vazi la kizalendo kabisa

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako