THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu wanne wa Jeshi la Polisi
Tanzania.
Aidha,
Rais Kikwete amefanya uteuzi wa nafasi za madaraka katika Jeshi hilo kufuatia
mabadiliko ya muundo wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es salaam leo, Jumanne, Desemba 3,
2013 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka waliopandishwa vyeo kuwa
Kamishna wa Polisi (CP) na ambao wote
walikuwa ni Naibu Kamishna wa Polisi ni DCP
Ernest Mangu, DCP Thobias Andengenye,
DCP Abdulrahaman Kaniki na DCP Hamdan Omari Makame.
Rais
pia amempandisha cheo SACP Athuman
Diwani kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.
Walioteuliwa
katika nafasi za madaraka katika Jeshi la Polisi ni CP Clodwing Mtweve ambaye anakuwa Kamishna wa Fedha na Utaratibu wa
Ugavi na Usafirishaji wa Watu na Vitu (Logistics),
CP Paul Chagonja ambaye anakuwa
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Isaya Mungulu ambaye anakuwa Mkurugenzi
wa Uchunguzi wa Makosa ya jinai (DCI),
CP Mussa Ali Mussa ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Jamii.
Wengine
ni CP Hamdan Omari Makame ambaye
anakuwa Kamishana wa Polisi, Zanzibar; CP Ernest Mangu ambaye anakuwa
Mkurugenzi wa Usalama wa Jinai, CP
Thobias Andengenye ambaye anakuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, CP Abdulrahman Kaniki ambaye anakuwa
Kamishna wa Uchunguzi wa Ushahidi wa Jinai na CP Abdulrahman Diwani ambaye anakuwa Naibu Mkurugenzi wa DCI.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
3 Desemba, 2013
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako