A

A

Sankara: Aliingia Ikulu kwa risasi, akatoka kwa risasi-2


Kwa ufupi
Wiki iliyopita tuliona jinsi aliyekuwa Rais wa Burkina Faso, Thomas Sankara alivyotengeneza mageuzi makubwa nchini mwake katika kipindi cha miaka minne kama kiongozi wa nchi, kabla ya kupinduliwa na kuuawa.
Wiki iliyopita tuliona jinsi aliyekuwa Rais wa Burkina Faso, Thomas Sankara alivyotengeneza mageuzi makubwa nchini mwake katika kipindi cha miaka minne kama kiongozi wa nchi, kabla ya kupinduliwa na kuuawa.
KUUAWA:
Pamoja na mikakati yote hiyo, Rais Sankara aliishia kupinduliwa na kuuawa kinyama pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Chama cha Council of Popular Salvation. Endelea
Rais wa sasa wa Burkina Faso, Blaise Compaore ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Sankara na waliofanya pamoja mapinduzi ya kumng’oa Rais Jean-Baptiste Ouedraogo, ndiye mhusika mkuu wa mauaji ya Sankara.
Nchini Burkina Faso, inaeleweka wazi kuwa Rais Compaore alishiriki kikamilifu mpango mzima wa kuuawa na kisha kupinduliwa kwa rafiki yake Sankara.
Sankara pamoja na maofisa wengine 12 waliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la askari waliokuwa na silaha, Okotba 15, 1987, ambapo baada ya kuuawa alizikwa kwenye kaburi ambalo lilishaandaliwa siku moja kabla.
Kuna maelezo mengi yametolewa kuhusu namna Compaore alivyomgeuka Sankara na kumuua, ingawa mwenyewe mara kwa mara amekuwa akisema wazi kutohusika katika mpango huo, lakini akikiri kuwa kuuawa kwa Sankara ni ‘makosa’.
Imeezwa pia kuwa, uhusiano mbaya kati ya Utawala wa Sankara na nchi jirani, ulikuwa miongoni mwa sababu za kupinduliwa na kuuawa kwake, huku Dikteta wa zamani Liberia, Charles Taylor naye akitajwa kuhusika.
Msomi mwanauchumi wa Liberia, Byron Tarr aliandika katika Jarida la Academic Journal la mwaka 1993, jinsi Taylor alivyokuwa na urafiki wa karibu na Compaore kabla ya kuuawa Sankara.
Awali, Taylor alitoroka jela ya Boston, Massachusetts nchini Marekani na kukimbilia nchini Ghana wakati huo ikiwa chini ya Rais Rawlings na kufungwa kwenye jela za nchi hiyo.
Rais Rawlings hakuwa tayari kumtoa Taylor kwa Marekani alikotoroka gerezani au nchi yake ya Liberia iliyokuwa chini ya Rais Doe. Inadaiwa kuwa, Compaore alikwenda Ghana na kukutana na Rawlings na kumwomba amwachie Taylor, ombi ambalo lilikubaliwa.
Kuachiwa kwa Taylor kunaelezwa kuwa ndiko kulikozaa mpango mzima wa kupinduliwa Sankara kwa msaada wa Libya, madai ambayo yalithibitishwa pia na Mke wa Sankara, Mariam Sankara. Taarifa zingine zinadai kuwa, Taylor alipelekwa kwenye mpaka na nchi ya Ivory Coast na kuachiwa huru, ambapo kukutana na viongozi wa kijeshi wa Libya waliomtambulisha kwa Compaore.
Vilevile, uchunguzi usio rasmi unaonyesha kuwa Ghana ilimwachia huru Taylor wakati tayari mauaji ya Sankara yameshafanyika.
Tume ya Haki za Binadamu ya Shiriki la Kutetea haki la Umoja wa Mataifa, liliitaka Serikali ya Burkina Faso kuchunguza sababu na wahusika wa mauaji ya Rais Sankara na familia yake kupewa taarifa. Hatua hiyo ilikuja baada ya familia ya Sankara kulalamika kutofuatiliwa kwa makini sababu za kuuawa kwake wachukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika. Hata hivyo hakuna aliyekamatwa kama mhusika wa moja kwa moja.
Compaore ndiye Rais wa sasa wa Burkina Faso tangu mwaka 1987, akishinda pia viti vya uchaguzi wa rais nchini humo kwa mara nne; 1991, 1998, 2005, na 2010.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako