Aidha amesema anayetaka kusaidia anaweza kupiga simu 0755061588 kwa maelekezo zaidi.
Naye
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Benedict Ngaiza ambaye
hospitali yake kwa sasa ndiyo inamtunza mtoto huyo amewataka wanawake
kujiepusha na vitendo vya ukatili hasa kwa watoto kwa kujiunga na uzazi
wa Mpango.
Akimwakilisha
Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Peter Kiula,amesema vitendo vya ukatili dhidi ya
watoto vina zidi kukithiri na anaamini inatokana na wanawake kubeba
Mimba bila Maandalizi.
Naye
muuguzi Anna Chaula katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma amewaomba wana
wake kushirikiana na Vyombo vya Dola kumbaini mama aliyemtupa Mtoto kwa
kuwa wanao fanya vitendo hivyo ni wale tunao ishi nao.
Naye
Makamu mwenyekiti wa Mtandao wa Police wana wake, mkoani Ruvuma Fadhila
Chacha amesema Mtandao wa Police wanawake unaendelea kupambana na
vitendo vya ukatili,Ndiyo Maana kila wakati huokoa uhai wa watoto.
Mkoa wa
Ruvuma wakati ukiwa katika kilele cha siku 16 za kulaani vitendo vya
ukatili dhidi ya mama na Mtoto tayari watoto watatu wameokotwa jalalani
na mmoja kuliwa na mbwa eneo la mfaranyaki baada ya kutupwa .
CHANZOhttp://songeahabari.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako