Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akiwasili kwenye ofisi yake iliyoko karibu na Ikulu mara
baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu
alikopokea tuzo ya uongozi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuja
kumpokea tarehe 19.12.2013
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maua kutoka kwa Mwenyekiti wa wake
wa viongozi, Mke wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa
William Lukuvi na Mwakilishi kutoka ofisi ya WAMA, mara baada ya
kuwasili ofisini hapoakitokea Dubai kupokea Tuzo ya uongozi itolewayo na
Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA akiangalia ngoma za utamaduni mara baada
ya kuwasili kwenye viwanja vya Ofisi za WAMA, ambako mamia ya wananchi
walikusanyika kwa ajili ya kumpongeza baada ya kurudi na Tuzo ya
uongozi aliyopokea huko Dubai tarehe 18.12.2013.
uongozi aliyopokea huko Dubai tarehe 18.12.2013.
Baadhi
ya wananchi walioshiriki mapokezi ya Mama Salma wanaonekana
wakimsikiliza wakati alipokuwa akiwahutubia katika viwanja vya WAMA
tarehe 19.12.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi waliofika kumpokea
aliporejea kutoka Dubai tarehe 19.12.2013. Mama Salma alienda huko
kupokea Tuzo ya uongozi ulitukuka kutokana na kazi anazofanya kupitia
Taasisi yake kwa ajili ya elimu kwa wanaotoka katika mazingira magumu,
afya ya mama na mtoto pamoja na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akiongea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Raymond Mushi wakati wa
shamrashamra za kumpokea Mama Salma baada bya kuwasili nchini akitokea
Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kupokea TUZO ya uongozi uliotukuka.
Tuzo hiyo hutolewa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi,
(CELD).
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza na wananchi waliofika kumpokea kwenye ofisi za WAMA tarehe 19.12.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako