A

A

TASWIRA,COMRADE MWIGULU NCHEMBA ALIPOZUNGUMZA NA MAELFU YA WANANCHI GEITA MJINI,HAIJAWAHI KUTOKEA.

Mwigulu Nchemba akiwasili Uwanja wa MKutano Geita mjini.Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba yakiendelea kwa shamrashamra za kutosha.Hisia za Wananchi kwa Mwigulu Nchemba ambaye katika Bango moja wapo anasomeka kama SOKOINE WA PILI NCHINI TANZANIA.Sehemu ndogo tu ya Maelfu ya Wananchi waliofika Kumsikiliza mh:Mwigulu Nchemba.Kueleka 2015 haikukosa,Hizi ni hisia za Wananchi wanaokoshwa na Uchapakazi wa Mwigulu NchembaMwigulu akikaribishwa Geita kwa Mabango.Kiongozi wa ACT Kanda ya Ziwa(Mratibu) akitoa shukrani zake za dhati kwa Mwigulu Nchemba kwa namna alivyokuwa mfano kwa kutetea Masikini na Wanyonge ndani ya BUnge na Nje ya Bunge.Mkuu wa Mkoa wa Geita akisalimia wananchi (Mwanamama)Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Msukuma akizungumza na Wananchi wake kuhusu Kero mbalimbali zinazowakumba ndani ya Mkoa wa Geita,Kubwa likiwa Wazawa kutopewa kipaumbele kwenye Madini,Pia unyanyasaji kwa Wachimbaji wadogo.Comrade Mwigulu Nchemba wakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita wakati wa Mkutano hii leo.Comrade Mwigulu Nchemba mbaye ni Naibu katibu Mkuu CCM Bara akionesha Ishara ya Dole "Mambo Poa" wakati akiwasalimia wananchi wa geita hii leo.Tanzania Oyeeeeee,Hiyo ndio salamu ya Mwigulu Nchemba mara zote apandapo Jukwaani kuzungumza na Wananchi."Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hatu jazi nafasi,Tunatafuta Viongozi wenye uwezo wa kusimamia Halmashauri zetu za Vijiji,Mitaana Vitongozi ili ziweze kufanya kazi za Maendeleo kwa Uadilifu na Ufanisi wa hali ya Kuridhisha"Hii ni sehemu tu ya Maelfu ya Wananchi wa Geita waliofika Kusikiliza Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mwigulu Nchemba,Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Kero za Wananchi wa Geita.Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi kuchagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi kwasababu ndio wenye sera inayotekelezwa,Hivyo wanajua mahitaji ya Wananchi wao."Kuna Wananchi wanatamani sana kubadirisha Vyama kama Nguo,Kubadirisha vyama sio suluhisho la Kutatua kero za Maendeleo.Tujitahidi kufanya maamuzi yenye tija wakati wa uchaguzi,tuchague Viongozi imara na wenye nia ya kuwaongoza.Achaneni na kubadirisha vyama vya siasa"Kupanga ni KuchaguaNaibu katibu Mkuu akisisitiza kuwa hakuna atakaye ichafua Tanzania yeye akabaki salama,Hakuna atakaye Iba mali ya Umma akatembea kifua mbele.Wahujumu Uchumi wote wa Nchi hii waanze kujiandaa kisaikolojia.Muonekano wa Umati wa Wananchi waliotulia wakisikiliza hoja za Msingi kutoka kwa Mwigulu Nchemba.Comrade Mwigulu Nchemba akisisitiza Jambo kwa Wananchi wa Geita Mjini kuhusu Uchaguzi wa serikali za Mitaa.Sehemu ya Wananchi wakati wa Mkutano huo.Comrade Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Geita Mjini.MKutano Umeshamalizika na Wananchi wanarejea makwao.
Picha na Sanga Festo wa Habari Kwanza

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako