WAKATI
bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya
kuzomewa na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Wema Sepetu ‘Madam’
anaponda raha ya maisha nchini China, Amani lina full data.
Bebi wa mbongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ , Wema Sepetu ‘Madam’.
Chanzo
makini kilicho ‘kloz’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini,
kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache
kabla ya Tamasha la Fiesta, akiwa ameandamana na wanaume wawili, ambao
ni meneja wake, Martin Kadinda na Petit Man, wote wakiwa wamekaa daraja
la kwanza la dege hilo.
Chanzo
hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na
Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou
nchini humo, Wema na wanaume hao wawili walichukua vyumba katika Hoteli
ya Holiday Inn, inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China.
“Yaani Wema jamani ana mambo, inavyoonekana lile rhumba la wakati ule ameshalisahau, amesahau
kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia kapata pesa
anavyoitapanya ovyo mpaka roho inauma. Wewe fikiria mtu amekwenda
kuchukua vifaa vya biashara, unakwenda na hao wanaume wa kazi gani kama
siyo kupoteza fedha tu,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu ‘Madam’ akipozi.
Inadaiwa
kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi
kuliko yoyote duniani, ni ununuzi wa vipodozi, kwani ana mpango wa
kufungua duka kubwa katika eneo ambalo halijatajwa jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi
maisha ya starehe, wakila bata katika klabu mbalimbali za usiku, ambako
wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha.
“Kwa
matanuzi anayofanya kule, hata hiyo biashara aliyoifuata haina maana,
angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli, angetafuta tu hoteli ya
kawaida ili kubana matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa, sasa wewe
mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa, tena na wanaume wawili
wanakutegemea, hizo pesa si kuzitapanya tu jamani,” kilisema chanzo
hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako