Oscar Pistorius |
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka 5 baada ya kukutwa na hatia
ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa adhabu
hiyo imetolewa baada ya mwanariadha huyo kukutwa na hatia ya kuua bila
kukusudia.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo majira ya saa
mbili asubuhi, Jaji Thokozile Masipa,amesema adhabu hiyo ni changamoto
kwa mwanariadha huyo na kuongeza kuwa mahakama imelazimika kutoa hukumu hiyo
kwani imejiridhisha na kwamba maamuzi hayo yataleta usawa wa pande zote kwenye
kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako