Mgonjwa,
Mwalihoba Nyasa, anaye sumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya titi, sasa
ameanza kunyonyoka nywele zake kwa madai ya kukokosa chakula kutokana na
kutumia dawa kali lakini hapati chakula.
Mtoto
Josephiner Obeid aliypooza miguu ni miongoni mwa wagonjwa hao
wanaoteseka katika nyumba ya kulala wageni ya Bosco iliyopo Ilala
Mchikichini jijini Dar es Salaam kwa kukosa chakula kwa madai ya
kutelekezwa na Taasisi ya Redeso.
Mtoto
Lucy Angela ambaye anajisaidia kwa kutumia mpira baada ya kutobolewa
tumboni naye ni miongoni mwa wagonjwa hao wanaoteseka katika nyumba hiyo
ya wageni kwa kukosa chakula 'hakika ukikutana na ndugu zetu hawa
unaweza kutokwa na machozi kwani inauma na kutia uchungu'
Mama huyu naye yupo katika mateso hayo, hakika inaumiza.
Watoto hawa nao hawajui cha kufanya wapo katika mateso.
Dada huyu ambaye ni mgonjwa hana la kufanya zaidi ya kumuachia mungu. |
Ndugu
zetu hawa ambao ni wakimbizi kutoka Jamhuri ya Watu wa Congo (DRC),
ambao ni wagonjwa ambao wanadai wametelekezwa na Taasisi ya Msaada wa
Maendeleo ya Jamii (Rudeso), yenye makao yake Kinondoni, wakiwa nje ya
nyumba ya kulala wageni ya Bosco iliyopo Ilala Mchikichini Dar es Salaam
leo. Inadaiwa kuna zaidi ya wakimbizi 100 waliopo jijini wanaishi
katika mazingira ya shida baada ya kutelekezwa na taasisi hiyo.
Dotto Mwaibale
WAKIMBIZI
zaidi ya 100 wanaokabiliwa na magonjwa mbalimbali, wametelekezwa na
Taasisi ya Msaada na Mandeleo ya Jamii (Redeso) ambayo ni wakala wa
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), baadhi yao
wameanza kunyonyoka nywele kutokana na kukosa chakula, kwa muda wiki
moja sasa.
Mtandao wa www. habari za jamii.com leo
ulifanikiwa kuwatembelea wakimbizi hao ambao wapo katika Hotel
mbalimbali zilizopo Ilala na Kinondoni katika nyumba za wageni Eritex na
Bosco ambapo wamehifadhiwa hapo wametokea Kambi ya Nyarugusu Mkoani
Kigoma kwa lengo la kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti na mtandao huo wakimbizi hao ambao ni wagonjwa
walisema wamekuwa wanateseka kwa muda sasa jambo ambalo wanaliona kuwa
linahatarisha maisha yao.
Walisema
pamoja na kutoa taarifa kwa wahusika ambao ni Redeso hadi sasa
hawajapatiwa msaada wowote hivyo kujikuta wakinywa dawa bila kula
chakula hali ambayo inawaletea madhara.
Mgonjwa,
Mwalihoba Nyasa, anaye sumbuliwa na ugonjwa wa kansa titi alisema
ameanza kunyonyoka nywele zake kwa madai ya kukokosa chakula kutokana na
kutumia dawa kali.
"Hii
si afya yangu na sikuwa hivi siwezi kubeba chochote na afya yangu
imeendelea kuteteleka na nywele zangu zimeanza kunyonyoka kutokana na
kukosa chakula" alisema Nyasa.
Mmoja
wa wakimbizi hao alisema baadhi yao wanamagonjwa ya kansa, kupoza,
ukoma na magonjwa mengine ambayo ni hatari iwapo hakutakuwa na utaratibu
mzuri wa kuwapatia chakula ili dawa ziweze kufanya kazi.
Baadhi
ya wakimbizi hao ambao ni wagonjwa ni Sango Nyasa (36), Josephiner
Obeid (15), Kashindi Alfan (47), Andhurin Elisha (5), Muhambo Msana (7),
Maulid Yunus (5), Jane Kabeza (30), Lucy Kashindi (11) na Mwalihoba
Nyasa (37) ambaye anasumbuliwa na kansa ya titi.
"Jamani
tunaomba msaada kwani hali zetu ni mbaya mmoja wetu ameshapoteza maisha
kutokana na tatizo hilo tunaomba msaada hata kwa serikali ya Tanzania,"
alisema.
Aidha
alisema wanawaomba wasamaria wema wengine kujitokeza kuwasaidia msaada
wa chakula kwani kwa sasa hawakopeki kutokana na kukosa fedha.
Alisema
wanapaswa kupata shilingi elfu 70 kila mmoja kwa wiki kwa ajili ya
chakula lakini hali hiyo imekuwa kinyume kwa takribani wiki nzima.
Mkimbizi huyo alisema iwapo hakuna juhudi ambazo zitachuliwa upo uwezekano mkubwa wakimbizi hao kupoteza maisha.
Akizungumza
kuhusu jambo hilo mmoja wa maofisa wa Taasisi ya Redeso, Neema Malulu
alisema yeye sio msemaji na kumtaka mwandishi awaulize UNHCR kwani wao
ndio wanatoa fedha.
"Mimi
sio msemaji, kazi yangu ni kuwapatia fedha wakimbizi hao baada ya
kupewa na UNHCR hivyo ni vema ukawaulize wao," alisema Malulu.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Ame Silima alisema
mimi ndio nampa taarifa hizo na kudai kuwa suala hilo linawahusu UNHCR
hivyo waulizwe wao.
"Upo
uwezekano wa kuwepo hapa kama ulivyosema ila wanao husika na watu hao
ni UNHCR nadhani itakuwa vema ukiwauliza wao kwanini hawawapatii chakula
wakimbizi hao," alisema Silima.
Jitihada
za kuwapata watu wa UNHCR kwa ufafanuzi ziligonga ukuta kwani kila
simu yao ilipokuwa ikipigwa walikuwa wahawapokei simu.
Ndugu
zetu hawa katika kupigania maisha yao awali walikuwa wakienda kukopa
vyakula katika maduka ya jirani na wanapoishi lakini baada ya kuona
hawalipi wenye maduka hayo wamesitisha kuwasaidia ambapo baadhi yao
wanadaiwa kuanzia shilingi 45,000 hadi 50,000.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako