Mwigulu: Tutalipa deni la Sh8.4 Tril
Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya
Dar es Salaam. Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).
Mifuko hiyo inaidai Serikali Sh8.43 trilioni. Mfuko wa PSPF unadai (Sh429 bilioni), PPF (Sh192 bilioni), NSSF (Sh467 bilioni), NHIF (Sh107 bilioni), LAPF (Sh170 bilioni) na GEPF (Sh6.8 bilioni).
Jumla hiyo ya deni la Serikali linahusisha deni jingine la PSPF la Sh7.06 trilioni ambayo ni malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema kuwa mifuko hiyo huikopesha Serikali kupitia wizara mbalimbali, fedha ambazo hutakiwa kulipwa baada ya muda fulani.
Alisema wizara zisipolipa na hivyo deni kukaa kwa muda mrefu, huingizwa kwenye deni la Taifa.
“Madeni hayo ni makubwa, yanahitaji baraza la mawaziri kujadili utaratibu gani utatumika kulipa,” alisema Mwigulu na kuongeza:
“Kwa mfano deni la PSPF ni kubwa na linahitajika kulipwa, hivyo tunaweka utaratibu lakini siyo kwamba Serikali hailip... kama mwaka jana tuliilipa PSPF zaidi ya Sh50 bilioni sema nao wana mahitaji yao.”
Akizungumzia deni la MSD, Mwigulu alisema: “Hili la MSD tumetaka mchanganuo wa wizara na kila halmashauri jinsi gani fedha zilizotolewa kwa ajili ya dawa, zimetumika”.
Alisema mwaka jana Serikali ilitoa Sh47 bilioni kwaajili ya dawa katika wizara na halmashauri, lakini fedha zilizotumika kununulia dawa ni Sh7 bilioni tu.
“Nyingine wamefanyia mambo mengine na ndiyo maana tunasema hatuwezi tukawa tunatoa tu fedha bila kupewa mchanganuo wa fedha hizo zimefanyiwa
[3:18PM, 28/10/2014] Sanga: Mwigulu: Tutalipa deni la Sh8.4 Tril
Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii.
Dar es Salaam. Serikali imesema inaandaa utaratibu wa jinsi ia kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).
Mifuko hiyo inaidai Serikali Sh8.43 trilioni. Mfuko wa PSPF unadai (Sh429 bilioni), PPF (Sh192 bilioni), NSSF (Sh467 bilioni), NHIF (Sh107 bilioni), LAPF (Sh170 bilioni) na GEPF (Sh6.8 bilioni).
Jumla hiyo ya deni la Serikali linahusisha deni jingine la PSPF la Sh7.06 trilioni ambayo ni malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema kuwa mifuko hiyo huikopesha Serikali kupitia wizara mbalimbali, fedha ambazo hutakiwa kulipwa baada ya muda fulani.
Alisema wizara zisipolipa na hivyo deni kukaa kwa muda mrefu, huingizwa kwenye deni la Taifa.
“Madeni hayo ni makubwa, yanahitaji baraza la mawaziri kujadili utaratibu gani utatumika kulipa,” alisema Mwigulu na kuongeza:
“Kwa mfano deni la PSPF ni kubwa na linahitajika kulipwa, hivyo tunaweka utaratibu lakini siyo kwamba Serikali hailip... kama mwaka jana tuliilipa PSPF zaidi ya Sh50 bilioni sema nao wana mahitaji yao.”
Akizungumzia deni la MSD, Mwigulu alisema: “Hili la MSD tumetaka mchanganuo wa wizara na kila halmashauri jinsi gani fedha zilizotolewa kwa ajili ya dawa, zimetumika”.
Alisema mwaka jana Serikali ilitoa Sh47 bilioni kwaajili ya dawa katika wizara na halmashauri, lakini fedha zilizotumika kununulia dawa ni Sh7 bilioni tu.
“Nyingine wamefanyia mambo mengine na ndiyo maana tunasema hatuwezi tukawa tunatoa tu fedha bila kupewa mchanganuo wa fedha hizo zimefanyiwa nini,” alisema Mwigulu.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako