MCHANA HUU BONGO LEAKS imepokea taarifa
za kusikitisha kutoka wilaya ya Mufindi zikihusisha Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kufukuzwa kutoka katika ofisi zake za wilaya zilizopo mjini
Mafinga.
Taarifa za uhakika kutoka kwa mdau wa
mtandao huu zimesema Chadema wamefukuzwa kutoka katika ofisi hiyo baada ya
kushindwa kulipa kodi ya pango kwa kipindi kinachodaiwa kufika miezi nane.
Mdau huyo amesema mkataba ulikuwa unakita
chama hicho kulipa Sh 80,000 kila mwezi na hivyo kufanya jumla ya fedha
wanazodaiwa kufikia Sh 640,000.
Jengo ambalo Chadema walipanga liko
upande wa pili wa stendi kuu ya Mafinga, karibu na kiwanda cha mbao
likimilikiwa na mama aliyetajwa kwa jina la Mama Rachel.
Mpaka tunakwenda mitambani taarifa kutoka
Mafinga zilikuwa zikionesha kwamba wafuasi wachache wa Chadema walijitokeza
katika ofisi hiyo kuhamisha baadhi ya mali za chama hicho na kung’oa bendera
yao.
Kama huo ndio ukweli, swali la kujiuliza hapa ni nani anayepaswa kulipa kodi za ofisi mbalimbali za chama hicho nchini?
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako