Jumapili iliyopita huko jijini Kigali nchini Rwanda mwanakaka Warren
Bright kutoka Tanzania alikuwa akifunga ndoa ya kimila na mpenziwe
mwimbaji sauti ya kwanza wa kwaya ya kwetu pazuri Ambassadors of Christ
aitwaye Claire Humure katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa binti
huyo na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutoka Tanzania na
Rwanda bila kusahau wanakwaya wa Ambassadors of Christ.
Harusi rasmi inatarajiwa kufanyika tarehe 17 mwezi huu katika kanisa la
kisabato la Ushindi jijini Dar es salaam. Bwana harusi ni kiongozi wa
kundi la Voices of victory la jijini Dar es salaam.
Jukwaa la maharusi nyumbani. |
Bwana harusi Warren mkono wa kuume akiingia na mpambe wake aitwaye Eric mwimbaji wa Ambassadors. |
Makaka wakimleta dada yao. |
Maharusi wakikumbatiana. |
Tukio la kuvalishana pete. |
Walipendeza sana, na eneo pia lilipendeza. |
Maharusi na wapambe wao. |
Wakiwa wamekaa kwa utulivu kabisa. |
Wakikumbatiana kwa furaha. |
Meza kuu safi kabisa. |
Waimbaji wa Ambassadors nao hawakuwa nyuma katika tukio hilo. |
Sarah akiwa sambamba na mwenzie kwenye harusi hiyo. |
Ambassadors of Christ wakiimba. |
Warren akianguka sahihi yake. |
Nyuso za furaha kutoka kwa maharusi na wapambe wao. |
Maharusi na wapambe wao. |
Maharusi na wazazi wao. |
Maharusi na waimbaji wa Voice of Victory pamoja na marafiki.©Kj Marcello & Warren Bright |
GK inawatakia maharusi maisha mema yenye furaha pamoja na kufanikisha tukio zima tarehe 17/08.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako