A

A

SERIKALI YAPOKEA MABEHEWA 25 YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 4.3 KUTOKA INDIA


 Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (kulia), akiangalia moja ya mabehewa kati ya mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni 4.3 aliyoyapokea kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industriles Limited ya India Dar es Salaam Leo, kwa ajili ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu.
 Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (katikati), akifurahia jambo wakati wa kupokea mabehewa hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.Shaaban Mwinjaka.
 Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu (mwenye tai kushoto),akimuelekeza jambo Waziri Mwakyembe.
 Waziri Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari wakati akipokea mabehewa hayo.
 Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
 Baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
 Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
 Waziri Mwakyembe akiangalia moja ya mabehewa hayo.
 Baadhi ya mabehewa hayo yakiwa yamepangwa katika njia yake bandarini baada ya kushushwa kutoka katika meli.
 Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Ephrahim Joel akikaza nati ya moja ya mabehewa hayo.
Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Francis Mpangala naye akikaza nati katika moja ya mabehewa hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa  habari za jamii.com.


Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imepokea mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni 4.316 kwa ajili ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industriles Limited ya India.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabehewa hayo Dar es Salaam leo, Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe alisema mabehewa hayo ni sehemu ya mpango kabambe wa Serikali wa kufufua Kampuni ya Reli Tanzania chini ya mapngo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa (BRN).

Alisema mpango wa BRN kwa Kampuni ya Reli Tanzania umelenga kuiwezesha kampuni hiyo kiutendaji ili iweze kusafirisha tani milioni 3.0 ifikapo mwaka 2016 kutoka tani 200,000 zilizosafirishwa mwaka 2012 kupitia Reli ya kati.

"Katika harakati za kufikia malengo haya makubwa, Serikali kupitia bajeti zake za mwaka 2012/2013 na 2014, ilitenga fedha kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali iliyolenga kuboresha vitendea kazi vya Kampuni ya Reli Tanzania" alisema Mwakyembe.

Alitaja miradi iliyopangwa ni  pamoja na kujenga upya vichwa vya Treni 8, kununua vinchwa vya treni vipya 13, mabehewa mapya 274 ya kubebea mizigo na mabehewa ya breki.

Mwakyembe alitaja mradi mwingine ni kununua mashine ya kushindilia kokoto, kununua mabehewa 22 mapya ya abiria na kununua mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto ambayo yamepokelewa jana.


Katika hatua hiyo Mwakyembe ametumia fursa ?hiyo  kuipongeza TRL kwa kupokea mabehewa hayo kwa wakati na kuishukuru Kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Limited ya India kwa utengenezaji wa mabehewa hayo kwa muda uliopangwa.


Alisema lengo ni kuiwezesha TRL kufikia malengo ya kusafirisha mizigo tani 3.0 na kutembeza treni za abiria tano kwa wiki ifikapo mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako