| Selemani Kiponda akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga |
| Kisha akakabidhi bendara ya chama hicho iliyokuwa imetundikwa nyumbani kwake |
| baadaye akatawazwa kwa kupewa kadi ya CCM na Diwani wa Kata ya Ihimbo,Hezron Nganyagwa (CCM) |
| Na kisha akapewa bendera ya CCM ili akaipandishe nyumbani kwake |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) mkoani Iringa kinazidi kubomoka pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa
na viongozi wake katika kukiimarisha.
Baada
ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema
Jimbo la Mufindi Kusini, Emanuel Ngwalenje hivikaribuni kutimkia Chadema
na wanachama wengine zaidi ya 100 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa
Iringa kwa nyakati tofauti walikikimbia chama
hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika tukio la juzi, Mwenyekiti Chadema
kata ya Ihimbo , Selamini Kiponda amekiongezea kidonda chama hicho baada ya
kujitoa na kuinga na CCM.
Kiponda alifikia uamuzi huo juzi kwa kile
alichosema amekuwa kiongozi wa Chadema kwa miaka minne na
ameweza kushawishi wakazi wengi katika maeneo mbalimbali katika kata ya Ihimbo
kujiunga na chama hicho lakini hawajawahi kupata ushirikiano wowte kutoka
uongozi wa mkoa na Taifa.
“Nilijiunga na Chadema mwaka 1993 wakati
ndio kwanza upinzani umeingia nchini na nimekuwa kiongozi kwa miaka zaidi ya
minne; hakuna ushirikiano wanachama wa Chadema huku vijiji tunahangaika kama
kuku wa kienyeji tusiyejua baba wala mama yetu, nimechoshwa na sasa nimeamua
kurudi CCM kwa kuwa ndio chama changu ambacho kwa kweli nilikuwapo tangu enzi
za TANU,” alisema.
Alisema kurudi kwake CCM kumechagizwa
zaidi na maendeleo yanayofanywa na diwani wa kata hiyo Hezron Nganyagwa pamoja
na mbunge wa Jimbo la Kilolo Profesa Peter Msolla.
Akimpokea mwanachama huyo, Katibu wa CCM Mkoa
wa Iringa, Hassan Mtenga alisema Kiponda amefanya maamuzi sahihi na kwamba
uamuzi wake unazidi kudhihirisha tofauti iliyopo baina ya vyama hivyo viwili.
Mtenga aliwaomba viongozi na wanachama wengine
wa Chadema wilayani Kilolo kufuata nyayo za Kiponda kwa kuachana na Chadema
inayohubiri vurugu badala ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako