Jinsi
teknolojia inavyokua kuna baadhi ya vitu kwenye miaka inayokuja
vitashindikana kufanyika kutokana na maboresho yanayofanyika
kuvidhibiti.
Unaambiwa kuna simu ya mkononi iliibwa lakini baadae
kidogo ikatuma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo kuonyesha
kuwa ndiye mmiliki wake.
BBCSwahili.com wameandika polisi katika eneo la Essex nchini
Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo aina ya HTC ambayo iliibwa
kutoka kwenye koti la mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea
nyumbani.
Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye
simu hiyo
ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza namba ya
siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.
Msemaji wa polisi alisema kuwa simu hiyo ilimpiga picha mwanaume huyu
alipojaribu kuingiza namba hiyo bila kufanikiwa ambapo email ya
Mwanafunzi huyo ndio ilituma ujumbe kwa polisi kuwataarifu kuhusu wizi
huo.