A

A

Sheikh Ilunga aaga dunia

Ilunga Hassan Kapungu
Ilunga Hassan Kapungu

SHEIKH Ilunga Hassan Kapungu ameafariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ugonjwa wa kisukari jijini Dar es Salaam. Mazishi yake yatafanyika leo Jumatatu saa 10 jioni. Mwili wa marehemu utasaliwa katika msikiti wa Kichangani, Magomeni-Mapipa jijini Dar.


Taarifa hii imetolewa na:
Sheikh Mohammed Kassim,
IPC Ubungo
Dar es Salaam

Sheikh Ilunga ambaye alikuwa mhubiri wa Kiislam nchini Tanzania na Afrika Mashariki,  aliwahi kukamatwa na Polisi na kufunguliwa mashtaka mwaka jana akiwa na viongozi mbalimbali wa kidini, wakituhumiwa kwa kosa la uchochezi wa dini kupitia kanda za CD na VCD wanazoziuza kwa waumini wao zinazoeneza chuki na ukabila ikiwemo kuhimiza kuwachinja mapadri.

Katika mtandao wa kijamii wa JamiiForums, baadhi ya wananchi wametoa maoni mchanganyiko kuhusu kifo hicho.