Ikiwa bado hakuna formula halisi ya kupenda mtu, na bado ni
kitendawili kuweza kutabiri mambo au matukio yanayoweza kutokea katika
mahusiano yenu hapo baadaye,basi mapenzi yatabaki kuwa ni moja ya jambo
lisilo tabirika, sababu ni vigumu kuweza kutabiri ni nini hasa kila
mmoja katika mahusiano anachowaza.Kama ilivyotokea kwa Diamond Platnumz,
hata baada ya kuachana na Wema kwa muda na kuendelea kutoka na watu
wengine, lakini mwisho wa siku amerudi kwa mpenzi wake wa zamani na hadi
hii leo bado wanadumu.Jambo ambalo lililomtokea Wema, ndio limemfika aliyekuwa mpenzi wa Linex, kwa kuomba kurudisha majeshi na kuwa kama zamani, bila kutegemea Linex aliamua kufika maamuzi ya kuvunja uchumba baada ya kukataa kwenda kuishi na mpenzi wake nje ya nchi, hivyo kuzua ugomvi mkubwa na kila mmoja akibakia kuchukua vya kwake hata baada ya kumvisha pete.
Hata hivyo mbali na kukaa single kwa muda mrefu, Linex aliwahi kukiri kuwa, bado anafikiria uamuzi wa kurudiana na mchumba wake huyo wa zamani, kwani si vibaya jambo hilo likitokea, na kukiri kuwa ni jambo la kwaida kwa wapenzi wa zamani walioachana kuweza kurudiana na maisha yakasonga.
Si jambo la kuona soo tena siku hizi pale mambo yatakapowashinda wawili waliotengana, kukiri makosa yaliyowahi kutokea hapo nyuma,kutatua na kuamua kurudiana. Mbona wengi tu imetokea, wakiwemo wasanii wengi tu maarufu wa muziki hapa Bongo kama Diamond Platnumz na Wema Sepetu, ambao hata wao ingawa bado hawajavalishana pete za uchumba, ila utasikia tu wakiitana yale majina kama wanayoitana baba na mama.