Zifuatazo ni kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali wa zile kamati
kwenye bunge la katiba linaloendelea sasa hivi hapa Dodoma ambapo viongozi hawa leo April 14 2014 wameendelea
kuwasilisha taarifa kutoka kwenye kamati zao,
Ni maoni ya pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga
mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo
wa serikali tatu.
Tundu Lissu: ‘Nusu karne ya
uongo iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na hakuwa na
mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya Tanzania
kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya muungano, nchi
hii ni haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii inahitaji
kuelezwa ukweli’
Mchungaji Mtikila: ‘tulijengwa
kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki hii nchi
yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, swala la muungano lilikua utapeli wa
kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika na Wazanzibari’
Mh Wassira: ‘Hati ya Muungano
ipo, naahidi kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa Mwenyekiti ndani ya
siku mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni kutaka kuvunja
muungano, je tume ingeyaleta? serikali 3 italeta mgongano’
Mh Wassira: ‘Katiba ya Znz ndio
itabakia kuwa sheria kuu kwa Znz kwa mambo yasiyokua ya muungano,
tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata matatizo,
itapunguzia Wazanzibari fursa’
Ismail Jussa: ‘Hoja za historia
kwamba tulikua vipi haziwezi kulibakisha taifa katika mgando, ukiangalia
katiba ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua Tanganyika na kuwepo
makamu wawili wa Rais’
Ismail Jussa: ‘Mkataba wa
muungano haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha kilichopo
ndani, ajabu bunge limefanya, tunapokua Znz tunasema mengine tukija huku
tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu’
Ismail Jussa: ‘Zanzibar
tumeachwa watupu, tumechoka na hatukubali tena, ktk mfumo wa serikali
mbili Zanzibar haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali kuendelea nao’
Ismail Jussa: ‘Kama kuna nia njema kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni Rais wa Znz kuondolewa kuwa makamu wa Rais’
CHANZO: MILLARDAYO.COM