A

A

Wema asema Kajala alimkwepa asimkumbatie akidai 'angemchafua', fedha ilinogesha urafiki na imeuvuruga

Wema asema Kajala alimkwepa asimkumbatie akidai

Urafiki wa Wema Sepetu na Kajala ulitajwa kuwa urafiki wa kweli hasa baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya shilingi milioni 13 ili asiende jela miaka 7, pesa aliyoitoa bure kumsaidia rafiki yake ambaye alimtaja kuwa ‘shujaa wa maisha yake’.

Hata hivyo, urafiki huo uliong’aa kama theluji ulipata doa na wawili hao waliripotiwa kuwa na bifu la chinichini ambalo lilijulikana baadae.
Wema Sepetu ambaye alishinda katika shindano la mrembo mwenye mvuto zaidi lililoendeshwa kupitia gazeti la Ijumaa la kampuni ya Global Publishers alifanya mahojiano na Global Publishers na kuweka wazi sababu zilizopelekea wawili hao waujunje urafiki wao.
Katika tukio la kwanza, Wema alieleza kuwa aliumia pale alipotaka kumuonesha upendo hadharani Kajala kwa kumkumbatia kwa shangwe walipokutana kwenye saloon moja Kinondoni muda mfupi kabla ya kwenda kwenye show ya Kigodoro Dar Live, lakini mambo yalikuwa ndivyo sivyo.
“Niliposhuka kwa ajili ya kuosha nywele nikamuona Kajala, kwa kuwa nilikuwa sijamuona muda mrefu. Nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye. Kweli nilipiga makelele ya furaha nilipomuona K, nikawa nakimbia kwenda kumkumbatia, kweli niliishiwa nguvu baada ya kunikwepa na kusema nooo… ‘Wema usinikumbatie’ na kuanza kutoa maneno ya dharau eti nitamchafua.” Wema amesimulia.
“Kusema kweli niliishiwa nguvu na kuona kama vile kizunguzungu huku aibu ikinijaa ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi. Basi huwezi kuamini, nilishindwa kujizuia na kujikuta nikimtukana, sikumbakisha. Wakati namtukana alikuwa amekaa kwenye kiti cha kuoshwa, nikaenda nikamsukuma na kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae mimi nioshwe, huwezi amini hali ya hewa ilibadilika kwani sikuwa na mudi tena.” Wema aliiambia Global Publishers.
Muigizaji huyo alielezea pia kuwa siku nyingine walikuwa safarini Arusha kwenye show ya Mirror na kwa kuwa yeye hakuwa na fedha mkononi zaidi ya ATM Cards, alimkopa Kajala shilingi laki mbili na elfu themanini.
Wema ameeleza kuwa Kajala alimpa fedha rafiki ndugu yake mwingine waliyekuwa nae ili akamuwekee bank kwa kuwa kuwa aliona Wema ameanza kukopa fedha zake na kudai kuwa aliandaa show huku akijua hana pesa. Sasa wakati wanaongea hayo, walikuwepo watu wengine watatu ambao walikuwa wanasikiliza. Baada ya muda Wema Sepetu hakumuona Kajala na ndugu yake na ndipo alipowauliza wale watu wengine na wao walimueleza walichokisikia kutoka kwa Kajala akimwambia ndugu yake huyo.
“Ndipo nikafungukiwa kuwa wananikimbia kisa nimemkopa K hizo laki mbili na elfu thamanini, kiukweli niliumia sana. Kanalalamikia laki mbili? Tena hakunipa alinikopesha? Nikajiuliza amesahau mimi nilitoa shilingi millioni 13 kumlipia faini asiende jela miaka saba? Nguo nikinunua nanunua sare, viatu sare, nywele sare, viatu sare, mapochi sare, ninachokula mimi na kunywa ndicho hichohicho. Siku zote alipokuwa gerezani nguo, viatu, hereni yaani kila kitu ilikuwa ni mimi, leo laki mbili na elfu thelathini niliyomuazima ananitangazia kwa watu? Iliniuma sana, basi palepale nikaenda benki nikatoa shilingi milioni mbili, nikamlipa fedha zake, nikakaa kimya nikajifanya sijui chochote kinachoendelea kwani ningefanya chochote ningeharibu show na kusingekuwa na maana yoyote ya sisi kwenda Arusha.”
Katika drama nyingine, Wema alieleza kuwa Kajala alikataaa kushiriki kwenye filamu waliyopanga kuchangia wote kiasi cha shilingi milioni 5 kila mmoja. Ameeleza kuwa wakiwa katika hatua za mwisho Kajala alimwambia kuwa anaenda China hivyo kama angetaka ashiriki basi ashuti vipande vyake. Hiyo kwa upande wa Wema iliielewa tofauti na hivyo akatafuta njia mbadala na kufanya filamu hiyo na Ant Ezikiel.
Credit: Global Publishers &Bongo5