Naibu Waziri wa Fedha(S)Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Balozi wa Tanzania hapa Washington DC Mh:Libereta Mulamula alipowasili Uwanja wa Ndege wa Washington DC.Wengine ni Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania hapa Washington,Wamwisho Kulia ni Mwenyekiti wa Shina la CCM Maryland Ndugu.Mrisho Mzese
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Balozi Bi.Libereta Mulamula wakwanza Kulia na Ndugu Mrisho Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Shina la CCM hapa MaryLand-Marekani.
Naibu Waziri wa Fedha(S) Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na DJ Luke wa Vijimambo(Kushoto) na Mrisho.
Furaha ya Watanzania Wanapokutana na Viongozi wao Nje ya Nchi ni Kujua hiki na Kile Kinachoendelea Nyumbani Tanzania,Hapa ni Habari za Bunge la Katiba,Uchumi n.k
Mh:Mwigulu Nchemba akijibu Maswali Kutoka kwa Mmoja wa Wanahabari wa Blog ya Vijimambo,Kubwa zaidi ni Kuhusiana na Swala la Uraia Pacha(Dual CitzenShip) ambapo Mh: Mwigulu Nchemba amesema "Naunga Mkono Swala la Uraia Pacha,na Chama Cha Mapinduzi kwenye Kitabu cha Maoni yake kwenye Rasimu ya Katiba Mpya waliweka Swala la Uraia Pacha na anaomba Wabunge Wenzake waliunge Mkono Swala hilo na Vile Vipengele Vyenye Kuhofiwa hasa Katika Chaguzi n.k Viangaliwe namna ya Kuviweka sawa ila Sio Kukwamisha Zoezi Zima la Uraia Pacha."
Mbali na hapo Mh:Mwigulu Nchemba akihojiwa na Vijimambo Blog amezungumzia Swala la Bunge la Katiba kuwa,Katiba Mpya Itapatikana endapo Waliopewa Kazi ya Kuitunga Wataacha tabia ya Kugeuza Bunge hilo ni Uwanja wa Siasa,Watachana na Kugeuza Bunge hilo Sehemu ya Kitega Uchumi,Mwisho Katiba Itapatikana Endapo Uzalendo Utawekwa Kipaumbele na sio Matakwa Binafsi".Hivi Karibuni Wajumbe kutoka CHADEMA,CUF NA NCCR na Wachache Kutoka Kundi la 201 Walisusia Bunge la Katiba kwa Madai Wamechoka Kusemwa Vibaya kwenye Bunge hilo,Kitendo hicho cha Kususia Bunge kimewakera Watanzania Waliowengi kwakuwa Sababu za Kususia Bunge hazina Uzito,Pia hii ndio fursa pekee kwa Watanzania kuandika Katiba inayokwenda na Muda na Mazingira ya Maisha yao,Hivyo Watu Wachache kutaka Kugeuza Bunge la Katiba Uwanja wa Kutafuta mtaji wa Kisiasa ni Kukosa Uzalendo kwa Taifa lao.
Picha/Maelezo na Festo Sanga-Washington DC