ARENA DE SAO PAULO.
Mechi sita zitachezwa katika uwanja huu uliopo mjini,Sao
Paulo.Umepewa nafasi ya kuchezwa kwa mechi ya ufunguzi itakayo husisha
wenyeji wa michuano, Brazil dhidi ya Croatia, Juni 12. Ni uwanja mpya
kabisa na utafunguliwa rasmi mapema mwaka huu. Unauwezo wa kuchukua
watazamaji wapatao 65, 867. Mechi nne za hatua ya makundi zitapigwa
katika uwanja huu, na nyingine mbili katika hatua za mtoano.
ARENA DA BAIXADA.
Ni uwanja unaoweza kuchukua watazamaji wapatao 41, 456. Upo katika
mji wa Curitiba, na ulifunguliwa rasmi mwaka 1914. Mechi ya kwanza
katika uwanja huu itakuwa ile kati ya Iran na Nigeria, Juni 16. Ni mechi
nne
tu zitachezwa katika uwanja huu, na zote zikiwa za hatua ya makundi.
tu zitachezwa katika uwanja huu, na zote zikiwa za hatua ya makundi.
MARACANA- RIO DI JANEIRO.
Wenyeji Brazil wanakumbukumbu mbaya na uwanja huu, walipoteza kwa
mabao 2-1 mbele ya Uruguay katika fainali ya mwaka 1950. Fainali ambayo
ilishuhudiwa na watu wapatao 200, 000, idadi kubwa zaidi ya
watazamaji katika historia ya soka. Kwa sasa, Maracana umepunguzwa ukubwa na kufikia kuchukua idadi ya watazamaji 76, 804. Mechi ya kwanza katika uwanja huu itakuwa ni ile kati ya Argentina na Bosnia,na unatarajia kutumika katika michezo saba.
watazamaji katika historia ya soka. Kwa sasa, Maracana umepunguzwa ukubwa na kufikia kuchukua idadi ya watazamaji 76, 804. Mechi ya kwanza katika uwanja huu itakuwa ni ile kati ya Argentina na Bosnia,na unatarajia kutumika katika michezo saba.
ESATADIO MINEIRAO- BELO HORIZONTE.
Uwanja huu una uwezo wa
kuchukua watazamaji wapatao,62,547.Ulijengwa
mwaka 1965, mechi ya Colombia na Ugiriki, itakuwa ya kwanza kupigwa
hapa. Mechi sita zitachezwa katika uwanja huu, nne za hatua ya makundi
na mbili za hatua ya mtoano.
ESTADIO NACIONAL DE BRASILIA- BRASILIA.
Uwanja huu ulifunguliwa rasmi mwaka 2012, una uwezo wa kukusanya
watazamaji 66,000. Mechi ya kwanza kuchezwa katika uwanja huu ni ile ya
Uswisi na Ecuador pia uwanja huu utatumika katika michezo saba sawa na
ule wa Maracana.
ARENA FONTE NOVA- SALVADOR.
Mechi kati ya Hispania na Uholanzi itachezwa katika uwanja huu, juni
13. Ni uwanja uliofungiliwa mwaka 1951 na una uwezo wa kuchukua
watazamaji wapatao, 48, 747. Utatumika kwa michezo sita.
ARENA PERNAMBUCANO- RECIFE.
Unatarajiwa kufunguliwa mapema mwaka huu, ukiwa na uwezo wa kuchukua
watazamaji wapatao 44, 248, Ivory Coast na Japan zinataraji kuamana
hapa, juni 14. Utachezewa kwa michezo mitano, minne ya hatua ya makundi
na mmoja wa hatua ya mtoano.
ESTADIO BEIRA RIO- PORTO ALEGRE.
Una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 48, 849 na ulifunguliwa
mwaka 1969. Mechi tano zitachezwa katika uwanja huu, nne za hatua ya
makundi na moja ya mtoano.
Viwanja vingine ni Estadio Das Dunas, uliopo katika mji wa
Natal.Uwanja huu unachukua watazamaji 42, 086, na mechi nne za hatua ya
makundi zitachezwa katika uwanja huo. Pia upo Arena da Amazonia,uliopo
katika mji wa Manaus.