April
17 2014 Wajumbe walio upande wa (UKAWA) kwenye bunge la katiba
wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba waligoma na kuamua kutoka nje ya
bunge hili hapa Dodoma baada ya Profesa Lipumba kumaliza kuzungumza
kwamba hawawezi kuendelea na bunge la matusi na ubaguzi.
Kingine kikubwa alichozungumza Prof. Lipumba ni
kusikitishwa na kauli
ya Waziri Lukuvi aliyoitoa kanisani weekend iliyopita kwamba jeshi
litatawala nchi ambapo April 14 2014 gazeti la Mwananchi lilimnukuu
Waziri Lukuvi akisema Kanisani ‘tukipitisha serikali tatu jeshi
litatawala nchi’
Kama hutoweza kusikiliza sauti yake hapa chini yafuatayo ni baadhi ya makubwa aliyoyazungumza leo asubuhi
‘Ni kweli kwamba kikao hichi nilipanga nisichangie kwa sababu niliona
mechi kali tukishindilia watu watakufa, sikusikia vizuri yaliyotokea
jana ila mimi sio mnafiki, nampongeza sana Mh. Mrema kwa hotuba yake
juzi, Mrema ndio mpinzani wa kweli, alisema angalia mambo yanayotokea
Znz msidhani yataishia Magogoni’
‘Baada ya hotuba ya Rais, mh. Seif Sharrif Hamad alihutubia, yeye ni
mchochezi wa hovyo kwa kumsingizia Rais, hakuna mtu yeyote anaweza
kunizuia kusema ninayoyaamini mimi, sio hapa wala mtaani, ni kweli
Jumamosi nilimwakilisha Waziri mkuu ambae hakunipa hotuba na mambo
yalinoga nikatawazwa kuwa chifu’
‘Viongozi wa dini waliliombea Bunge pale Kanisani, mimi Waziri nipo
pale… nisiongee chochote??!! tukiendeleza ambayo hayako kwenye mila zetu
Znz na Tanganyika inaweza kuwa kama Korea kaskazini na kusini, hofu
niliyonayo ni juu ya rasimu yenyewe kwa sababu kwanza imejengwa kwenye
misingi ambayo siiamini’
‘Zanzibar inatambulika kama nchi kwenye katiba yao toka hata kwenye
katiba ya nyuma kabisa, yapo mapungufu muundo wa serikali 3, ukisoma
rasimu wanasema serikali ya Tanganyika imevaa koti la muungano lakini
koti lenyewe tunapokezana, leo anavaa Mwinyi, leo anavaa huyu’
‘Hatujawahi kutoa bajeti inayotosha kwa jeshi la Wananchi, mmeshawahi
ona wanaandamana kudai haki zao? nina miaka zaidi ya 50 na nisingependa
kuiona Tanzania hii inakwenda kwenye maisha ambayo sikuyazoea ili
kuepusha haya tusijaribu tusichokijua, hii ni hofu yangu… hakuna wa
kunizuia kutoa hofu yangu’
‘Ukweli ni kwamba kama umesoma hii rasimu, muundo unaweza kuwa
umeandikwa vizuri lakini hauwezi kuwepo, Rais hakutoa vitisho bali
mawazo yake kama Mtanzania, hawa jamaa wamekubaliana, serikali ya Znz
wachukue CUF, bara CHADEMA na muungano waachiwe CCM’