Mfano
wa ramani ya Center inayotarajiwa Kujengwa ya Dr. Jakaya Kikwete
National Sports VillageMAANDALIZI ya ujenzi wa kijiji cha michezo...
MAANDALIZI
ya ujenzi wa kijiji cha michezo kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete
Sports Village yanaendelea vizuri, ambako tayari Ikulu, Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya Michezo wametoa baraka kijengwe
mjini Dodoma.
Akizungumza na Tanzania Daima,
Mratibu wa ujenzi wa kituo hicho, Wilhelm Gidabuday, alisema ujenzi wa
kituo hicho kikubwa na cha kwanza nchini, tayari maandalizi yake
yameshafikia pazuri na Ikulu ya Tanzania kupitia ofisi ya Katibu wa
Rais, imeshawapa baraka ya kutumia jina la Rais katika kituo hicho.
Gidabuday
alisema, wiki iliyopita walikutana na Katibu wa Rais, ambako
waliwasilisha maombi yao na kukubaliwa na kwamba, kuanzia sasa kituo
hicho ambacho ujenzi wake utasaidia kuinua vipaji vya michezo yote hapa
nchini, kitafahamika kama kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete (Jakaya
Kikwete Sports Village).
“Nidokeze tu
kuwa, mipango yote inakwenda sawa, tumeshafikisha ujumbe wetu Ikulu na
imekubalika, awali tulipanga kituo chetu tukiite John Steven Akhwari
Sports Village, lakini baada ya kukaa na Mzee Akhwari, kwa pamoja
tuliridhia kituo hiki kitumike kama sehemu ya kumpa heshima
Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village,” alisema Gidabuday.
Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village,” alisema Gidabuday.
Gidabuday
ambaye pia anaratibu mbio za Kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine,
Sokoine Mini Marathon, pamoja na matembezi ya amani kutoka Ujiji –
Kigoma mpaka Dar es Salaam, alisema wamepanga kutumia shughuli zote
mbili kuwafahamisha wananchi kuhusu umuhimu wa ujenzi wa kituo hicho
katika maendeleo ya sekta ya michezo na utamaduni hapa nchini.
Wakati huo
huo, waandaaji wa msimu wa pili wa Sokoine Mini Marathon,
zitakazofanyika Kijiji cha Monduli Juu, wametangaza rasmi sehemu ambako
fomu za ushiriki wa mbio hizo zitapatikana.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday,
alisema, fomu za ushiriki wa mbio hizo kwa mwaka huu zitapatikana
wilayani Monduli, katika Kijiji cha Monduli Juu.
CHANZO: Tanzania Daima