Kutokana
na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam pamoja na
kusababisha mambo mengi kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja
yanayounganisha njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.
Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha
familia kuhama kutoka kwenye makazi yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es
salaam inasema watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima
watano.
Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya
Dar es salaam amesisitiza
hali sio nzuri hivyo wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi
yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi
zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima barabarani.
Hizi ni baadhi ya picha kati ya nyingi zinazosambaa kwenye mtandao.