Licha ya kufunga mabao matano katika mzunguko wa pili wa
ligi kuu, Tanzania,mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania Prisons
ametupiwa lawama kuwa kupoteza kwake nafasi za kufunga magoli
kumechangia timu hiyo kuwa katika hatari ya
kushuka daraja.
” Peter ni mchezaji wetu, ni mfungaji wa kutegemewa katika timu
lakini hatoi mchango wa kutosha. Anapoteza sana nafasi, kitu ambacho
kimetugharimu katika michezo minne iliyopita”.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani kabisa ya timu
hiyo, Peter mwenye mabao tisa msimu huu ameambiwa anatakiwa kuongeza
umakini uwanjani ili kuinusuru timu yake isishuke daraja.
” Mwalimu ameliona hilo na kumtaka apigane kuisaidia timu. Kazi yake
ni kufunga magoli kitu ambacho ana uwezo nacho, ameambiwa kuongeza
umakini na kutumia vizuri nafasi anazopata.
Ligi imekuwa ngumu lakini ni uzembe wetu wenyewe tuliofanya katika michezo ya hivi karibuni iliyopelea hali hii”.