Wakati Top 20 za Kora awards zilipoanza wiki ya 10,
P-Square ndio walikua wanaongoza top 10 hizo huku Mwanamuziki Zahara
kutoka Africa kusini akishika nafasi ya pili na ya tatu kushikiliwa na
Amri Diab , muimbaji wa miondoko ya Rock kutoka nchini Misri. Kipindi
hiki cha wiki ya 10 Diamond Platnumz, alikua akishikilia nafasi ya 13
huku kukiwa na msanii mwingine kutoka Kenya yaani Redsan ambaye alikua
nafasi ya 19. Wiki ya 11 iliwaacha P-square wakipigwa na butwaa baada ya
kutupwa nafasi ya 12 huku Zahara akichukua namba moja na Amri diab
kutoka misri akishika namba 2.Wiki ya 11 ilishuhudia wanamuziki wawili
waliobakia kutoka Afrika mashariki wakiondolewa kwenye Top 20 hii.
Wiki ya 12 ilimrudisha Diamond Platnumz akishika nafasi ya 13 akiwa
msanii pekee kutoka
Afrika mashariki. Zahara, mwanadada kutoka Afrika
kusini aliyekua akishika namba moja alitupwa namba 8 akiachia namba 1
kwa Amri Diab na namba 2 kwa Aster Aweke, mwanadada kutoka
Ethiopia. Wiki ya 13 Diamond alishika namba 14 na cha kufurahisha ni
hatua ya Diamond kukamata namba 3 wiki ya 14 akiacha na Koffi Olomide na
ya kwanza kukamatwa na jamaa yuleyule kutoka Misri alieshikilia nafasi
hiyo tokea wiki ya 12.
Kwa matokeo haya ya KORA awards ni wazi kwamba Diamond Platnumz ndiye
msanii anayekubalika Afrika Mashariki na anaweza kuwashangaza wengi kwa
tuzo anazoweza kuzichukua .Mahali tuzo hizi zitakapofanyika haijapagwa
bado lakini ni kati ya Benin, Cote d’Ivoire, Ethiopia na South Africa.
Kama wewe ni mpenda muziki una kila sababu ya kum-support Diamond
Platnumz na kumuwezesha kuchukua tuzo za Kora kwa mara ya kwanza.