Meneja wa Manchester City,Pellegrini
anaamini kuwa itakuwa inasikitisha sana kwenye soka kama Chelsea
wanashinda taji la ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Man City na vinara wa ligi,Liverpool wamekuwa
wakifunga sana kuliko kikosi cha
Jose Mourinho msimu huu huku Pellegrini
akionyesha wazi kukerwa na staili ya uchezaji ya timu hiyo ya Stamford
Bridge.
Liverpool wamefunga magoli 90 ya ligi katika michezo 33 msimu huu na Man City wakifunga magoli 84 katika michezo 31.
Wakati Chelsea wakiwa wamefunga magoli 65 katika michezo yao 33 na
Pellegrini anahisi kuwa timu inayoshinda taji inatakiwa iwe bora zaidi
kuliko rekodi kama hiyo.
Huku akisema,”Itakuwa inaumiza sana kwenye soka,kwa mashabiki na kwa
kila mmoja.Nafikiri kuwa mpira wa kuvutia zaidi,magoli mengi unayoweza
kufunga,yanatakiwa kutunukiwa”
Pellegrini akaongeza kuwa,”Sisemi kuwa sio muhimu kulinda vizuri.Soka
ni kushambulia na kuzuia.Lakini nafikiri timu kubwa lazima zicheze kama
timu kubwa.”
Pia raia huyo wa Chile,alionyesha kutokubaliana na Mourinho na meneja
wa Liverpool,Brendan Rodgers kwa kupinga kwao kutokuwepo kwenye mbio za
ubingwa.
Na kusisitiza kuwa,”Sifikiri ni kweli.Labda wanajilinda mapema kama watakosa kushinda taji.”
“Lakini ukweli,sifikiri kama mameneja wote wawili wanahisi hilo ni
sahihi.Kazi hii ni kuhusu presha.Siwezi kuamini kuwa katika kazi hii
kubwa bila ya kuwa na presha.Na muhimu zaidi pale unapoiongoza timu
muhimu na ikiwa na nafasi ya kushinda taji.”
Pellegini akaendelea kwa kudai,”Sifikiri nini wachezaji wao
wanafikiri lakini na uhakika kama ningesema kwa wachezaji wangu kuwa
hatuna presha yeyote kushinda,sifikiri kuwa hilo lingefanya kazi.”
Mwisho akasema kuwa hafikiri kama wachezaji wanakubali hilo na sio
wachezaji muhimu ambao hawana nafasi ya kushinda taji.Tena wakiwa nyuma
kwa pointi moja au mbili dhidi ya vinara huku akisema labda wakiwa nyuma
kwa pointi 10.
Na kusema hafikiri kama wachezaji wa Chelsea au Liverpool wanaamini hawana presha ya kushinda taji.