A

A

MUME WA MTU AFA AKIWA NA MKE WA MTU


Mwili wa marehemu Vedasto Ager ukiwa kwenye jeneza tayari kwa kuagwa.NI gumzo la aina yake ndani ya mji wa Kibaha mkoani Pwani ambapo mume wa mtu aliyejulikana kwa jina la Vedasto Ager (43) amefariki dunia baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari aina ya Fuso akiwa amempakiza mke wa mtu kwenye pikipiki.

Kifo cha Vedasto kilichotokea Aprili 6, mwaka huu kimeacha maswali kibao kutokana na muda
wa tukio hilo kuwa usiku wa saa saba.

Mwanamke huyo alijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa chanzo kimoja, marehemu Vedasto alikuwa akifanya kazi ya kuuza tiketi kwenye mabasi yaendayo mikoani huku mwanamke huyo akifanya kazi ya kuuza chakula ambayo ni maarifu kwa jina la Mama Lishe.


Ndugu na jamaa wa marehemu Vedasto Ager wakiuaga mwili wa marehemu.

Uwazi lilifika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao walisema
hakuna anayejua kuwa wawili hao walikuwa wakitokea wapi kwani wote walikuwa mbali na maeneo wanayoishi! “Hata sisi tunashangaamarehemu alikuwa amembeba mke wa mtu saa saba usiku
wakitokea wapi kwenda wapi?” alihoji mkazi mmoja.

Uwazi lilipata bahati ya kuzungumza na mume wa majeruhi huyo, Fautunatus Simon ambapo alisema: “Mimi nilikuwa napita, ghafla niliona ajali.


Nilipokwenda pale nilikuta kila mtu ameanguka kivyake. Nilipowaangalia vizuri nikagundua mmoja ni mke wangu akiwa na Vedasto. “Vedasto alifariki dunia palepale lakini mke wangu alikuwa ana majeraha, hatua ya kwanza niliwakimbiza Hospitali ya Tumbi nikishirikiana na wananchiwengine.


Waombolezaji.

Vedasto aliingizwa mochwari lakini mke wangu alipelekwa Muhimbili.” Akizungumzia tuhuma za marehemu kuwa na uhusiano na mke wake, mume huyo alisema hata yeye amezisikia na akasema atamuuliza mkewe akipata nafuu. “Binafsi marehemu nilikuwa namfahamu sana lakini sijapata ukweli kuwa usiku ule walikuwa wanatokea wapi?” alisema.


Marehemu Vedasto Ager enzi za uhai wake.

Kamanda wa Polisi tukio hilo. “Gari lililosababisha ajali hiyo halijapatikana lakini polisi wanaendelea na upelelezi,” alisema.