Iliwachukua dakika nane tu mabingwa wa Ulaya kuchomoa bao hilo, mfungaji Bastian Schweinsteiger aliyemalizia kazi nzuri ya Mario. Mandzukic dakika ya 66.
Mapema kipindi cha kwanza, Danny Welbeck alikosa bao la wazi akiwa yeye na kipa Manuel Neuer akaokoa, wakati kabla ya hapo alimnawisha mpira Javi Martiezn na kufunga bao ambalo lilikataliwa na refa.
Mshambuliaji wa Bayern Bastian Schweinsteiger alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei kwa kumchezea rafu Rooney.
Kwa matokeo hayo, United sasa inahitaji ushindi katika mchezo wa ugenini Aprili 9, mwaka huu.
Katika mchezo mwingine wa Robo ya michuano hiyo usiku huu, Barcelona ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid Uwanja wa Camp Nou.
Diego Coasta alitangulia kuifungia Madrid dakika ya 56 Gabriel ‘Gabi’ Fernandez Arenas, kabla ya Neymar da Silva Santos Junior kuisawazishia Barca dakika ya 71 pasi ya Andres Iniesta.
Barca sasa inahitaji ushindi katika mchezo wa marudiano ugenini Aprili 9, mwaka huu.