Askari wa Mataifa Mbalimbali waliojumuika na Watanzania Kusherekea Miaka 50 ya Muungano Kutoka Kushoto ni Nigeria,Poland,Zimbabwe na Zambia waki kwenye Picha ya pamoja na Mh:Mwigulu Nchemba
Kushoto ni Ndugu Mrisho Mzese Kutoka Maryland na Ndiye Mwenyekiti wa Shina la CCM Maryland.
Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea Kusalimiana na Watanzania Mbalimbali walofika kwenye Ukumbio wa Marriott Hotel hapa Washington DC kusherekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Askari wa Jeshi kutoka Ubalozi wa Nigeria aliyefika Kujumuika na Watanzania kwenye Sherehe za Muungano wa Miaka 50 wa Jamhuri ya Muungano Ya Tanzania.
Watanzania wakiwa Kwnye Mavazi ya Kiafrica zaidi
Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 zimefana sana hapa Washington DC.
Tanzania ianapendwa sana na Mataifa Mengine ya Africa,Kushoto ni Raia wa Nigeria na Kulia ni Raia wa Cameroon wamefika Kuungana na Watanzania hapa Washington DC kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na hawa Wazungu waliopata Kuishi Nchini Tanzania miaka ya 1990's.
Tanzania Is All about kwa hapa Washington DC,Tuudumishe Muungano Wetu.
Huyu Dada wa Kitanzania amesafiri Kutoka Calfoni hadi Washington Kwaajili ya Kuuongoza Watanzania kuimba Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Marekani,Ameonesha Kipaji chake cha ajabu cha Kuimba Nyimbo zote mbili kwa Ustadi Mkubwa sana.
Balozi Libereta Mulamula akiwa na Mme wake alipomuita Kwaajili ya Kumtambulisha kwa Watanzania waliofika kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
Viongozi wakisikiliza Kwa Makini maneno ya Balozi Mulamula(hayupo Pichani).
Mmoja ya Viongozi wa Serikali ya Marekani akifurahia Umoja na Urafiki wa Tanzania na Marekani kidiplomasia,Na ameomba uendelee Kudumishwa.
Hapa akitosi Glasi na Balozi Mulamula Kuonesha Upendo na Mshikamano Miongoni Mwa Watanzania na Serikali ya Marekani.
Mh:Mwinyohaji Makame akizungumza n Watanzia hapa Washington DC kuhusu Umuhimu wa Muungano Kwa Wananchi wa Zanzibar,Amesisitiza Watanzania Wajikite kujadili maswala ya Maendeleo na sio Kuongeza Idadi ya Serikali kitu ambacho kinapoteza Muda na hakina Manufaa kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza n Watanzania na Wananchi wa Mataifa Mbalimbali waliofika Kusherekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania,Mh:Mwigulu amesema ni Wajibu kwa Kila Mmoja wetu katika Kizazi hiki kuandika historia ya kipekee kwa Kuulinda na Kuudumisha Muungano wetu kwa Miaka 50 zaidi,Kizazi kijacho kitawahukumu Watanzania endapo Muungano Utavunjika kwa Sababu tu ya Kupenda Vyeo na Ukosefu wa Utashi wa Kisiasa.
Watanzania hawa Wakipata UKODAK kwenye sherehe za Muungano hapa Washington DC.
Nafasi ya Kupata Ukodak na Mh:Mwigulu na Mke wake(Kushoto).
Viongozi wa Chama Cha mapinduzi Kutokea TEXAS.

Mh:Mwigulu Nchemba akiingia na Mh:Balozi Libereta Mulamula kwenye Usiku wa Muungano hapa Washington DC.

Mc akiendesha Shughuli kwenye USiku wa Miaka 50 ya Muungano.

Usiku wa Muungano Umefana sana,Watanzania wapo Wamoja.

Tutaulinda Muungano Wetu.

Watanzania Wanaipenda Tanzania yao.
Viongozi wa Mataifa Mbalimbali katika Picha ya Pamoja na Balozi Libereta Mulamula,Mh:Mwigulu Nchemba na Mh:Mwinyihaji Mara baada ya Mh:Mwigulu NChemba kumaliza Kuzungumza na Watananzania.
Safu ya Viongozi wa Jumuia za Watanzania kwenye Majimbo mbalimbali hapa Marekani wakiwa katika Meza ya pamoja na Mh:Balozi Mulamula na Mh:Mwigulu Nchemwa wakati wa Usiku wa Muungano hapa Washington DC.


Sehemu ya Umati wa Watanzania waliofika Kwenye Usiku wa Muungano hapa Washington DC.

Usiku wa Muungano Ulipambwa na Nyimbo za Kitanzania tu,Hapa Mziki unaendelea Kusherekea Miaka 50 ya Muungano Wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akizunguma na Watanzania Kwenye Usiku wa Miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC.Mwigulu amezungumzia Kuhusu Uraia Pacha na Kuwaahidi Watanzania Kuungana nao Kuipata haki hiyo Kikatiba na Chama cha Mapinduzi kimependekeza hilo kwenye Rasimu ya Katiba Mpya,Pia amezungumzia Sababu za Kiuchumi kuhusu Mzigo wa Serikali ya tatu inayopendekezwa na Rasimu huku akiwapa Uhuru Wataanzania Kutafakari kwa Kina kuhusu Jambo hilo,na Mwisho amezungumzia kuhudu dhamira ya Wazi ya UKAWA kuvuruga Mchakato wa Katiba,na dhamira hiyo imepangwa kutoa awali wakati wa Ukusanyaji wa Maoni na hata Kwenye Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la katiba.Hivyo Kususia kwao Bunge ni jambo walilopanga na Wamelitekeleza.Mh:Mwigulu amepeleka pongezi kwa Watanzania Wote kwa Kupuuzia Kitendo hicho walichokifanya UKAWA kwsababu hakikuwa cha Kizalendo na Kimelenda Kuligawa Taifa.
Picha/Maelezo na Sanga Festo-Washington DC
26/04/2014