Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria
sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika
kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi
mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria
sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Muungano.
Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
Kikosi cha Wanamaji
Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais
katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha Maadhimisho ya
miaka 50 ya Muungano.
Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
Maandamano ya Pikipiki.
Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.