Famous celebrity couple inayo-hit sana hapa town, Wema
Sepetu na Diamond Platnumz kutarajia kufunga ndoa na kuwa mume na mke
mwishoni mwa mwaka huu, hii ni kutokana na mtabiri maarufu kutoka nchini
Tanzania.
Yahya Hussein ni mtabiri maarufu mwenye makazi yake jijini Dar es
salaam na amefanikiwa kutabiri mambo mengi sana kuhusu wapendanao hao,
Yahya Hussein anatabiri kuwa ifikapo mwezi wa nane mwaka huu,wawili hao
watakuwa mume na
mke,aliongezea nakusema kuwa inabidi wahakikishe harusi
hiyo inafanyika la sivyo, itawabidi wasubiri hadi mwaka 2016 tena mwezi
wa nane.
“Ndoa yao inabidi ifanyike katika mwaka unaogawanyika kwa mbili” alisema Hussein.
Diamond Platnum na Wema Sepetu wameweza kupitia mengi sana katika
maisha yao ya mahusiano, hadi kufikia kuachana na baadae, walirudiana
mapema baada ya Diamond kuachana na celebrity mwingine maarufu kama Dvj
Penny, mtabiri huyo anatabiri kuwa vikwazo vengi vitazidi kutokea katika
mahusiano yao, nakuwashauri kuvumilia hayo yote yajayo na kukaa pamoja
waweze kuyapita yote hayo.