TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHADEMA yamshukuru Rais Kikwete kwa maendeleo
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wilaya ya Karatu katika Mkoa wa Arusha.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wilaya ya Karatu katika Mkoa wa Arusha.
Aidha,
chama hicho kimempongeza Rais Kikwete kwa kusambaza maendeleo kwa
Watanzania wote bila kujali msimamo wao wa kisiasa na hata katika maeneo
yanayounga mkono upinzani.
Shukurani
na pongezi hizo zimetolewa mchana wa leo, Jumanne, Aprili 22, 2014 na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mheshimiwa Lazaro Titus
Massey wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la
Halmashauri hiyo mjini Karatu. Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na CHADEMA.
Halmashauri hiyo mjini Karatu. Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na CHADEMA.
“Ni
lazima tutoe shukurani nyingi kwako Mheshimiwa Rais kwa sababu bila
wewe kuwa Rais wa Tanzania sisi Karatu tusingepata jengo hili. Pamoja na
kwamba Halmashauri yetu ni CHADEMA bado umeamua kuchangia sana
maendeleo ya Wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo
hili. Sisi hata robo ya fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” amesema Mheshimiwa Massey huko akishangiliwa na wananchi.
Jengo
la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu limegharimu kiasi cha shilingi
bilioni 1.412 na kati ya hizo, Serikali imetoa shilingi bilioni 1.394 na
Halmashauri imechangia shilingi milioni 18 tu.
Akizungumza
baada ya kumsikiliza Mheshimiwa Massey, Rais Kikwete amesema kuwa ni
sera ya Serikali yake kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila
kujali misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na
ukweli kuwa kila Mtanzania anataka na anayo haki ya kupata maendeleo.
“Sisi
hatuna wasiwasi, wananchi wa Karatu wamechagua CHADEMA lakini chama
hiki hakina Serikali. Wananchi wamechagua chama bila Serikali.
Halmashauri mnayo lakini Serikali tunayo sisi. Katika kusambaza
maendeleo, sisi hatuwezi kubagua. Hiyo ndiyo demokrasia na Serikali yetu
inaheshimu sana demokrasia na misingi ya utawala bora,” amesema Rais Kikwete.
Wakizungumza
baadaye kwenye mkutano wa hadhara wabunge wote wawili wa CHADEMA,
waheshimiwa Cecilia Paleso na Israel Nanse wamerudia tena kumpogeza Rais
Kikwete kwa kusambaza maendeleo katika maeneo yote ya Tanzania yakiwemo
yaliyoko chini ya wapinzani.
“Chini
ya uongozi wako, maendeleo yamesambazwa na sisi Karatu tumenufaika
sana. Ni matumaini yetu kuwa chini yako, tutaendelea kunufaika na sera
zako sahihi,”amesema Mheshimiwa Paleso.
Naye Mheshimiwa Nanse amesema: “Mheshimiwa
Rais sisi kwetu hapa hatuna ugomvi kati ya vyama vya siasa. Siye
CHADEMA tunajua kuwa CCM ni chama tawala Tanzania na CHADEMA ni chama
kiongozi hapa kwetu Karatu. Ni uhusiano huu uliowezesha Karatu kuendelea
kupata maendeleo.”
“Tunakushukuru
na kukupongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuifungua nchi yetu kwa
barabara kila mahali. Aidha, sisi wana-Karatu tunakushukuru sana kwa
mradi wa maji ambao umeuzindua leo”. Tunakushukuru sana.
Rais
Kikwete alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Karatu, Mkoa wa
Arusha na kesho atafanya ziara ya Wilaya ya Mwanga katika Mkoa wa
Kilimanjaro.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu- Dar es Salaam.
22 Aprili,2014