DEREVA mmoja wa pikipiki 'bodaboda'
yenye namba za usajili T 555 CFE ambaye jina lake halikufahamika mara
moja amevunjika mguu baada ya kugongana na gari aina ya Toyota Land
Cruiser lenye namba DFP 9597 mkoani Morogoro. Ajali hiyo imetokea
barabara ya zamani ya Dar es Salaam jirani na stendi ya daladala katika
Manispaa ya Morogoro mapema leo.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)