April
16 2014 saa saba kasoro mchana makamu mwenyekiti wa bunge la katiba
hapa Dodoma aliwasha kipaza sauti na kuzungumza kuhusu matangazo mawili
yaliyomfikia, moja la wageni na la pili ni la hati ya muungano ambayo
hatimae imepelekwa bungeni baada ya kuzungumziwa sana na Wajumbe
mbalimbali hasa wanaotaka uwepo wa serikali tatu waliosema hati hiyo
haipo.
Makamu Mwenyekiti alisema ‘nimepokea hati ya
makubaliano ya muungano
na ni certified copy na sasa nampa dakika mbili Mh. Wassira atoe maelezo
ya hati hii’
Mh Wassira akaanza >>
1.
Juzi nilisimama katia bunge hili na kusema kwamba hati ya muungano
iliyokua inapigiwa kelele sana, ipo katika hali nzuri na ndani ya siku
mbili itafikishwa bungeni.
-
Sisi wote tumeapa na mwisho wa kiapo chetu tukasema ewe Mungu
nisaidie, Mungu wa madhebu yote ni Mungu wa ukweli na uongo ni kazi ya
shetani, wamegawana kabisa Mungu wa ukweli na Shetani wa uongo.
-
Baada ya hati kupatikana jana Tundu Lissu na wenzake wamekutana
wakazungumza kwamba sasa tusema sahihi ya Karume sio sawa, tunaipeleka
wapi Tanzania? yani kila siku uongo unataka utawale Tanzania na ukweli
upuuzwe?
-
Watanzania tujihadhari sana na Mawakala wa shetani maana Mungu
anatumia Wanadamu kufikishia ujumbe wake kwa Wanadamu wengine na Shetani
anatumia Wanadamu pia, lazima tukwepe mamlaka ya shetani na Mawakala
wao.
-
Mh. Tundu Lissu amewakashifu waasisi wa taifa Mzee Karume na Mwl.
Nyerere Mungu awaweke mahali pema, anasema ni madikteta na waongo…. mimi
nasema heshima ya viongozi wetu waasisi hailindwi na vyama, italindwa
na Watanzania wote, wajibu wa kulinda heshima yao ni wa wote.
-
Hatuzuii mtu kusahihisha sera lakini huwezi kusema viongozi wetu wale
walikua ni waongo na Madikteta, hatuna haki ya kuwakashifu, namwambia
rafiki yangu Tundu Lissu, ulinzi wa heshima ya viongozi hawa ni wa
Watanzania na utalindwa kwa gharama yoyote.