Wizara
ya maliasili na Utalii imemfuta kazi mkurugenzi wa bodi ya utalii
Tanzania dokta Aloyce Nzuki kwa kutokuwa na imani nae pamoja na utendaji
usioridhisha.
Hii
imekuja baada ya kikao cha pamoja kati ya Bodi hiyo na waziri wa
maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu ambao waliketi pamoja na kutathmini
utendaji kazi ya Mkurugenzi huyo.
Waziri
NYALANDU amekiri kupokea Changamoto kadhaa zinazokwamisha ufanisi wa
majukumu ya Bodi ya Utalii katika kusimamia Sekta hiyo na kusema ‘mimi
na Naibu waziri wangu nimeridhika na kuridhia kuondolewa kazini kwa
Aloyce Mzuki’
Kwenye
sentensi nyingine Waziri Nyalandu amesema ‘sisi kama Wizara tutampangia
kazi nyingine, vilevile nimeiagiza bodi ya utalii Tanzania waitangaze
nafasi ya Mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii nchini’
Mwingine
aliezungumza ni mwenyekiti wa bodi hiyo Balozi Charles Sanga aliesema
sekta ya utalii inahitaji mabadiliko makubwa katika kufikia azma ya
Serikali ya kuongeza idadi ya watalii nchini kuliko taifa lingine lolote
barani Afrika.
Kwa sasa nafasi hii ya mkurugenzi itakaimiwa na Devotha Mdachi ambae ni mkurugenzi wa masoko katika bodi.