Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za mastaa wa muziki Drake na Rihanna kwamba wamerudisha uhusiano wao wa kimapenzi.
Ingawa wawili hao waliopachikwa jina la ‘AubRih’ (Kwa maana ya Aubrey
na Rihanna) mpaka sasa wamekuwa wakisisitiza bado ni
marafiki wa
kawaida, headlines zao za hivi karibuni zinaonyesha kuna kitu zaidi ya
urafiki kati yao.
Rihanna amekuwa akionekana na Drake wakiongozana kwenye ziara ya
kimuziki ya Drake Ulaya ambapo kwa mara ya kwanza walionekana pamoja
nchini Ufaransa, kisha Ujerumani na jana usiku walionekana pamoja jijini
Manchester – England.
Na hizi ni picha za ushahidi wa wawili hao walivyokuwa wakijiachia kwenye mitaa ya jiji la Manchester usiku jana.