WASANII wawili wa muziki wa kizazi kipya nchini Omary Nyembo 'Ommy
Dimpoz' pamoja na Vanessa Mdee wamefanikiwa kumshawishi msanii wa
kimataifa Victoria Kimani kutengeneza 'collabo'.
Wasanii hao wamefanikiwa kumshawishi msanii huyo, kutokana na kazi zao wanazozifanya na mashabiki wao wanavyozipokea.
Akizungumza katika moja ya mahojiano aliyoyafanya alipotembelea nchini
hapa kwa mualiko maalumu, Kimani alisema kuwa amefikiria kufanya nyimbo
na Vanessa Mdee kutokana na umahiri wake pamoja na ubunifu alionao.
Alisema kuwa anahitaji mtu mwenye sifa kama za Vanessa hivyo, kukutana
na msanii huyo kumezidi kuimarisha dhamira yake ya kufanya muziki na
msanii huo na kuamini kuwa utakuwa ni miongoni mwa muziki utakaofanya
vizuri katika soko la muziki nchini.
"Naamini Vanessa ni msanii mzuri, tena anauwezo mkubwa hivyo akifanya
kazi na mimi nyimbo hiyo itavunja rekodi mbalimbali na itatikisa katika
ngazi za kimataifa na soko la muziki" alisema Kimani.
Alisema kuwa kwa upande wa Ommy Dimpoz pia anahitaji kufanya naye
collabo, ambapo itaongoza idadi ya wasanii watanzania kufanya naye
nyimbo akiwemo AY .