Shangwe za GK leo zipo kwa mwalimu Christopher na Diana Mwakasege ambao
mwezi huu basi wamefikisha miaka 30 ya ndoa yao. Ambapo kulikuwa na
tafrija fupi ya kusherehekea tendo hilo iliyofanyika jijini Arusha wiki
iliyopita ambayo ilihudhuriwa na mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri
nchini Askofu dkt Alex Gehaz Malasusa, familia ya mwalimu Mwakasege,
ndugu, jamaa pamoja na marafiki. Mungu aendelee kuwainua watumishi hawa
ambao wamekuwa baraka kwa taifa letu la Tanzania. GK inawapongeza sana
na kuwatakia maisha marefu zaidi ya ndoa pamoja na baraka zitokazo kwa
Mungu ziambatane pamoja nanyi siku zote mkazidi kupata maarifa zaidi
katika kuwahudumia watu wake.