Picha juu haihusiana na ajali iliyotokea.
Habari zilizotufikia hivi punde ni
kwamba treni ya mizigo imepata ajali eneo la GodeGode mkoani Dodoma.
Mtu mmoja anasadikiwa kufa huku wengine watano wakiwa hawajulikani
walipo. Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba Treni hiyo ilisombwa na
maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Juhudi za
kukinasua kichwa cha treni bado zinaendelea. Kwa habari zaidi na picha
tutakuletea hivi punde.
Chanzo : ITV TANZANIA