Kama
hii ilikupita, ilikua wakati wa mechi ya South Africa vs Brazil
iliyochezwa Johannesburg South Africa ambapo wakati wachezaji wapo
uwanjani, alijitokeza mtoto ambae ni shabiki wa Neymar na kutaka kwenda
kukutana na staa huyu ila walinzi walimzuia.
Hata hivyo juhudi za walinzi hazikufanikiwa kwani tayari Neymar
alishajua akaamua kumfata na
kumpeleka mtoto huyu kwa wachezaji wengine
wa Brazil ambao walicheza nae kidogo, kumbeba na kumpiga picha na Neymar
picha ambayo ilipigwa na David Luiz.
Unaweza kutazama video ya huyu mtoto kwenye mwisho wa hii post ambapo
mechi hii ilikua mechi ambayo Brazil walishinda 5-0 huku Neymar
akiondoka na hat trick.
Kama
unataka usipitwe na stori kama hizi, ungana na millardayo.com na kuwa
mwanafamilia kwenye facebook, twitter na instagram kwa jina hilohilo la
MillardAyo.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako