A

A

Jihadhari na mtego huu wa kuiba password ya Facebook

via Evarist Chahali @ blogu ya KULIKONI

Jana nilifahamishwa na rafiki yangu mmoja kwamba ametumiwa barua pepe inayoonyesha kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa huko Tanzania. Katika e-mail hiyo, mwanasiasa huyo anaonekana kulalamika kuhusu chapisho (post) lililowekwa na rafiki yangu huyo (japo hakuna chapisho aliloweka).

Ni kwa namna gani matapeli (hackers) hao hujaribu kukutega (trick) wapate password yako? 

Matapeli hao wanakupa link wanayodai ndiyo yenye chapisho (post) lako huko Facebook. Ukiibonyeza link hiyo, inakutaka u-login kwenye akaunti yako ya Facebook. Kimsingi link hiyo sio ya Facebook bali inalenga kunasa password yako.

Mara nyingi matapeli hucheza sana na hisia za mlengwa wao. Kwa mfano, katika mbinu hii wanafahamu kuwa pindi ukipata e-mail inayokulaumu kwa kosa mbalo hujalifanya, ni rahisi kukurupuka kwa hasira kwa nia ya kutaka kumthibitishia huyo anayekutuhumu kwamba, hujafanya kitu kama hicho.

Tahadhari muhimu kuhusu hackers ni kwamba pindi upatapo e-mail za ‘kisanii’ kama hiyo aliyotumiwa rafiki yangu, IFUTE HARAKA SANA. Usihangaike kuwajibu kwa sababu unapo-reply e-mail kuna taarifa fulani kwenye “full header” inayoweza kumpatia hacker taarifa za kukuhujumu.