STAA
wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amejikuta akikumbuka pete
aliyovishwa na aliyekuwa mchumba wake, marehemu Saidi Banda ‘Max’ na
kusema ataendelea kumuombea kwani alikuwa ni mwanaume aliyekuwa na
malengo makubwa kwake.
Mainda
alifunguka hayo kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema kuwa kila
akiziona picha za siku alipovishwa pete ya uchumba, anajikuta akitokwa
na machozi.
“Miaka inakimbia sana miss u so much...! Kama ndoto vile, siku ile sitaki kuikumbuka ila kwa yote namshukuru Mungu.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako