Tofauti na unavyoweza kufikiri, mrembo huyu ameenda shule na ana fani
muhimu. Mbali ya kuwa model, Corazon ni mwanasheria; kitu ambacho
nimekipenda sana kwa sababu kuu mbili.
1. Kuna tabia/kasumba ya kuamini kuwa warembo wanaopenda au kufanya
modeling ni mambumbumbu. Hii sio kweli. Wengi wanapenda tu (hobby au
passion) na haina uwiano wowote na uwezo wa kiakili au busara. Natumaini
wengi wetu tutafikia mahali tukaelewa hili. Mfano mwingine ni Flaviana Matata ambaye alisomea uhandisi (engineering;) kitu ambacho baadhi mnaweza kuwa hamfahamu na mkashangazwa.
2. Fundisho kwa madogo wanaofuatia nyuma kuwa hata kama unapenda kuwa
mchezaji, model, au mwanamuziki, hiyo sio sababu ya kukacha au kutokuwa
makini na shule. Unaweza kufanya yako, kama modeling, na bado ukapiga
kitabu. Ambao mlizaliwa kabla ya awamu za Jakaya nadhani mnaweza
kukumbuka Leodgar Tenga alipokua anapiga soka Yanga na Taifa Stars na
wakati huo huo akiwa mwanafunzi Chuko Kikuu Dar (UDSM)
Picha na BuoArt. kwa picha za models zaidi, tembelea BuoArt kwenye Facebook>>facebook.com/buoart