Refa
Andre Marriner huenda akawekwa kando kwenye michezo ya mwishoni mwa
juma baada ya kufanya makosa ya kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji wa
kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Arsenal na Chelsea ambapo Chelsea
ilishinda 6 bila.
Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa
siku ya Jumamosi baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kushika mpira, lakini
Kieran Gibbs alipewa kadi nyekundu na kuondolewa kimakosa.
Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa kuwa yeye ndiye
aliyeshika mpira, hata hivyo uamuzi wa awali ndio ulikua wa mwisho.
Hata hivyo baadaye Mariner alikiri na kuomba radhi kwa makosa
yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa
katika mchezo huo.
Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa kimesema kuwa matukio ya
kumwadhibu mchezaji kimamkosa ni nadra kutokea na mara nyingi
husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi
SOURCE:BBC