"Mechi ambayo siwezi kuisahau katika maisha yangu ni ile ya Simba dhidi
ya Zamalek, kule Misri. Ukitoa maandalizi yetu kuelekea katika mchezo
ule. Wachezaji tulifanya kazi kubwa uwanjani. Mechi ilikuwa ngumu tangu
mwanzo na jamaa ( zamalek) wakapata bao ila maajabu mwamuzi alikataa.
Ilikuwa katika dakika kama ya 23 hivi, Matola alijifunga wakati
akijaribu kuzuia mpira wa krosi. Ilikuwa ni maajabu waarabu kukataliwa
bao katika uwanja wao. Tukajua ilikuwa ni nafasi yetu. Hatukupata muda
wa kupumzika uwanjani. Muda wote tulikuwa tukikimbizwa. Walipopata bao
tukajiambia wasipate lingine. Tukafika katika mikwaju ya penati tukiwa
hoi, ila tukashinda mechi. Zamalek Vs Simba, 2003 ni mechi ngumu kuwahi
kucheza katika maisha yangu ya soka " - ATHUMAN MACHUPPA AKIZUNGUMZIA
MCHEZO WA SIMBA VS ZAMALEK
Credit Shaffihdauda
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako