A

A

CCM Wahitimisha Kampeni Zao Kalenga kwa Kishindo

Katibu Mkuu CCM,Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga wakiingia kwenye Uwanja wa Mkutano Kata ya Nzihi Jimbo la Kalenga,Pia walichukua muda kusalimiana na Wananchi wa Kata ya Nzihi waliokuwa na Shauku ya Kusikia maneno ya Viongozi hawa wa Chama Cha Mapinduzi.Mapokezi Mazito ya Mgombea wa CCM Ndugu Godfrey William Mgimwa wakati wa Kufunga Kampeni hapa Kalenga hii leo.Katibu Mkuu CCM akifurahia Jambo na
Naibu katibu Mkuu-CCM Bara Mh.Mwigulu Nchemba na Mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa.Msanii Dokii ambaye ni kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi akiimba wimbo maalumu unaomuhusu Mgombea wa CCM Jimbo La Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa na anavyotakiwa Kutatua changamoto za Wanakalenga na Kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kama alivyokuwa Mbunge wa CCM aliyefariki.Chifu Mkwawa akizungumza na Wananchi wa kata ya Nzihi,Kubwa amewaomba Kumpigia Kura Godfrey William Mgimwa Kwa sababu yeye Kama Chifu amekuwa bega kwa bega na Chama Cha Mapinduzi na ameshuhudia Maendeleo Makubwa yakifanywa na  CCM hususani Ujenzi wa Hostel za Wasichana Mashuleni,Umeme,Vituo vya AFya na Barabara zinazopitika wakati wote.Mh.Kangi Lugola akiwaomba Wanakalenga Kumchagua Godfrey WIlliam Mgimwa hapo Kesho kwasababu ni Kijana na ananidhamu,Amesema hahitaji kuona Wananchi wanapoteza Muda kuchagua watu wanamtusi Rais wa Nchi,Wanatoka Bungeni wakati wa Bajeti na Wamegeuza chama cha Ukoo.Katibu wa UVCCM Taifa Ndugu Sixstus Mapunda akiwahakikishia Wanakalenga Usalama wao katiaka Zoezi Zima la Kupiga Kura.Katibu wa CCM Mkoa Wa Mtwara Ndugu.Akwilombe akitoa wito kwa Wanakalenga kuacha kusikiliza Propaganda eti Godfrey William Mgimwa anarithi Ubunge.Amewambia Godfrey amepatiakana katika Mchakato halali wa Kura za Maoni tena ukihusisha wagombea 9.Wale wanaosema Kuwa Mgimwa anarithi Ubunge ni Waongo kwa sababu wao Wenyewe Chama Kizima ni Mtu na Mdogo Mtu au Mkwe na Mkwe au Baba na Mtoto(ameorodhesha U-familia ndani ya Chadema).
Naibu katibu Mkuu CCM-Bara Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Kata ya Nzihi hii leo wakati wa Kufunga Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.
 Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh.Mwigulu Nchemba amewasihi Wanakalenga(kata ya Nzihi)Kuendeleza Wembe wa Kuikataa CHADEMA kabisa kabisa katika Nchi hii kwasababu wamekuwa Vinara wa Kusababisha Mauaji na Machafuko ya Amani katika Miji yetu.Pia amesisitiza kuwa Uchaguzi huu Mdogo haubadirishi Serikali,Kwasababu wenye Ilani ni CCM na Ilani Inayotekelezwa Kalenga niya CCM,Ametolea Mfano kuwa Itawekazana Vipi Amefariki Muumini wa Kiislamu eti Unamwita Askofu akaendeshe Mazishi,au Amefariki Mkristo unamuita Shekhe akaendeshe Misa ya Mazishi??.Ni jambo lisilowezekana hata kidogo,CCM ndio wenye Ilani Inayotekelezwa hivyo Mbunge anayetakiwa kusimamia Ilani hiyo ni Godfrey William Mgimwa wa Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu CCM Taifa Kanali Mstaafu Kinana akifunga rasmi Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi,amewaomba sana Wanakalenga keuendelea Kuwa na Imani na Chama Cha Mapinduzi na Kesho Wananchi wajitokeze wakapige Kura kumchagua Godfrey William Mgimwa iliaendelee kutekeleza pale alipaochia Mbunge aliyefariki.
Picha na Maelezo na Sanga Festo wa Habari Kwanza Media/Blog