Mtalaka ambaye ni Raia wa Uingereza Amanda Rodgers
ametoa kali ya mwaka baada ya Kufunga Ndoa na Mbwa wake kipenzi
aliyempa Jina la Sheba baada ya kudai kuwa na mapenzi ya dhati na Mbwa
wake huyo kwa muda mrefu sasa.
Amanda Rodgers ameolewa na Mbwa wake huyo (Sheba ) katika harusi iliyofana kwa namna ya kipekee huko Nchini Croatia katika hafla iliyohudhuriwa na watu takribanni 200.
Mtalaka huyo wa miaka 46 aliyekuwa amevalia kigauni
chenye rangi nyeusi huku bwana harusi ambaye ni mbwa akiwa amevalia
Shela Jeupe. Wapendanao hao walionekana kuwa na Nyuso za furaha huku
Amanda Rodgers Akisisitiza kuwa Aliamua kufanya Uamuzi huo baada ya
Kutengana na mumewe wa Ndoa miaka 20 iliyopita.
Amanda Rodgers Akiwa na Mumewe Sheba |
“Mbwa huyu(Sheba) Nimekuwa nae Maishani kwa
kipindi kirefu sana, yeye ndiye ambaye ananifanya nicheke, nifurahi na
kunituliza pindi ninapojisikia vibaya”